Makala: Yaliyomuweka shimoni Antonio Conte mpaka sasa

PITCOL

Senior Member
Joined
Aug 8, 2017
Posts
128
Reaction score
66
Kiukweli kama kuna kocha ambae analala bila kujua kesho yake ataamkaje yani kama bado yuko katika kibarua basi ni muitaliano Antonio Conte kocha mkuu wa Chelsea kwa sasa. Yuko na wakati mgumu kutokana na kutopata matokeo mazuri yani timu imekuwa haina consistency kulinganisha na msimu uliopita, Historia ya mmiliki wa timu ndiyo inamuukumu Conte na kumpa wakati mgumu sana. Akiwa na msimu wake wa pili Chelsea na pia akiwa ndie bingwa mtetezi wa EPL inaonekana kabisa hawezi kutetea ubingwa huo tena.

Tunajaribu kuangalia tu baadhi ya mambo ambayo pengine yamechangia kwa namna moja au nyingine Conte kutoka kuwa kocha bora wa EPL mpaka kufikia kuishi kwa mawazo kila siku. Baadhi ya mambo hayo ni kama yafuatayo:-

1:Kutopata wachezaji alio wataka waje.
Mwalimu wakati mwingine anaona kabisa kutokana na haina ya uchezaji wake basi kuna baadhi ya wachezaji akiwapata wanaweza kumfikisha pale anapopataka. Conte aliwataka sana Romelu Lukaku,24, pamoja na Alex Sandro,27, kutoka Juventus. Ilikuwa ni majira ya kiangazi lakini watu hawa hakuwapata kwani Lukaku alitimkia zake Man U dakika za mwisho kabisa kwa ada ya £75m. Ilimfanya akamchukua Morata kutoka Madrid mtu ambae aliwahi kufanya nae kazi Juve lakini hakuwa na uzoefu wowote ktk EPL na bado anaonekana kupata wakati mgumu.
Ishu ya beki wa kushoto Sandro kutoka Juve ni kwamba walishindwana bei hasa ukizingatia kuwa soko la sasa hata beki tu anauzwa mpaka £75m. Majira ya baridi akamtaka sana Edin Dzeko kutoka Roma lakini wakashindwana katika mambo binafsi hasa muda wa kukaa Chelsea. Hii ilimfanya kumchukua Olivier Giroud kutoka Arseanal ikionesha kuwa ana pata watu wale ambao hakuwataka kwa wakati husika.

2:Kuachana na Diego Costa & Matic pasipo watu sahihi.
Hawa wote yani Diego Costa pamoja na Nemanja Matic ni wachezaji wenye kariba ya do or die yani kufa na kupona wakati wanaipigania timu yao. Watu waliokuja kuziba nafasi zao {Morata na Bakayoko} wanaonekana kabisa hawana hiyo mentality. Iki ni kitu ambacho Chelsea wana kikosa sana kwa sasa kutokana na wakati mgumu wanao upitia. Kante mwenyewe hawezi kupambana kama wapambanaji wenzie wanakosa hali ya kutaka kufia kiwanjanai.

Ukweli binafsi nilimuunga mkono Conte kwa sababu alikuwa anajaribu sasa kuendelea kutengeneza timu yake na siyo kutembelea viatu vya mwingine. Lakini namna Conte alivyo achana na Diego Costa sio namna ya uprofessional, Conte alimtumia sms Costa na kumwambia kuwa hayupo katika mipango yake ya msimu ujao. Kibaya zaidi akamuuza Matic kwa maadui zake katika ubingwa japo mchezaji mwenyewe hakuwa na nia ya kutaka kutimka Chelsea.

3:Kubadili mfumo wake mama uliompa mafanikio.
Niliwahi kusema hapahapa katika moja ya makala zangu kuwa moja ya vitu vilivyo mwangusha Pep Guardiola mwaka jana ni pamoja na kuto kuwa na mfumo rasmi. Mwaka huu kasimama na mfumo wake mama wa 4-3-3 na ana kula maisha tu. Antonio Conte alikuja na mfumo mzuri sana katika EPL wa 3-4-3 mfumo ambao baadhi ya makocha walionekana kuukubali na kuanza kuutumia muda mwingine akiwemo mzee Wenger na Guardiola.

Mfumo huu ulimpa mafanikio sana Conte kiasi cha kushinda mechi 13 mfululizo za EPL. Baada ya kumuuza Matic na Costa, Conte akaamua kubadili mfumo. Sasa amekuwa akipenda kucheza sana na washambuliaji wawili yani 3-5-2 japo muda mwingine amekuwa akirudi katika mfumo wake mama. Bakayoko ameshindwa kuleta kitu ambacho Conte pengine alikitegemea na hivyo sasa kutokuwa na mfumo rasmi. Ishu ya mfumo inabaki palepale hata kama kuna ukosefu wa baadhi ya wachezaji katika kikosi cha kwanza yani first 11, Jurgen Klopp ana thibitisha hilo.

4:Kugombana na David Luiz
David Luiz anaitumikia Chelsea ikiwa ni katika kipindi chake cha pili baada ya Jose Mourinho kuwa amemuuza PSG. Conte baada ya kuja akasema hapana na kutokana na mfumo wake wa 3-4-3 akaona kabisa David Luiz ni mtu sahihi sana kwanza anaijua EPL na amewahi kucheza Chelsea. Kweli Luiz ni mtu kwani ana ku-offer vitu vingi, anapiga free kick, ana piga vichwa hasa mipira ya kona na mwisho wa siku anaweza kucheza kama kiungo mkabaji pale inapo bidi.
Huwezi kumlinganisha David Luiz na kijana aliyechukua nafasi yake kwa sasa Christensen ,21. Ikumbukwe tu baada ya Chelsea kufa 3-0 kule Roma katika ligi ya mabingwa ulaya hapo ndipo kutoelewana kati ya Conte na David Luiz kulipoanza. Conte akiona kuwa Luiz alikuwa ni
chanzo cha kichapo hicho na pia Luiz kukosoa mbimu za mwalimu huyo katika kipigo icho ikiwa mechi ya kwanza ilikwisha kwa goli 3-3 kule darajani.

Baada ya hapo David Luiz akatolewa katika kikosi cha kwanza na mpaka leo ana cheza zile mechi ambazo sio kubwa sana na akicheza kubwa basi ujue Christensen au nahodha Gary Cahill mmoja wao hapo anakosekana katika mechi iyo. Luiz alikuwa ana mchango mkubwa kwenye timu kulinganisha na mebeki wangine wote.

5:Wamesajili Quantity kuliko Quality.
Baada ya Antonio Conte kuonekana kuwa ana kosa usajili ule anaoutaka basi amekuwa akisajili tu wachezaji wa kutosha pengine ambao wana viwango wa kawaida sana. Chelsea sasa inaonekana kuwa na wachezaji wengi ambao wengi wao ni wakaida kuliko kuwa na wachezaji wachache ambao ni bora. Danny Drinkwater wa sasa sio yule ambae alikuwa kisu wakati Leicester City wanawashangaza wengi kwa kutwaa taji la EPL.

Watu kama Zappacosta, Giroud, Emerson, Bakayoko, Barkley wote hawa wanaonekana kuwa wachezaji wa kawaida. Ukweli ni kwamba kwa sasa kama unataka wachezaji bora kutoka kwa wakubwa wenzio na pengine kutoka kwa wale saizi ya kati {timu}basi lazima pesa za kutosha zikutoke. Soko la usajili ndipo hapo lilipo kwa sasa yani ukiitaji mshambuliaji wa kiwango basi kiasi cha pesa cha £70m+ lazima zikutoke. Kama utaona ni pesa nyingi basi utasajili wachezaji wengi ambao ni wa kawaida tu na sio bora.

Mwisho: Antonio Conte atafuata nyayo za watu kama akina Ancelotti ,Di Mateo na makocha wengine pale Chelsea. Ni vigumu kuamini kuwa msimu unao kuja kama bado tutabaki na Conte Chelsea. Mtu kama Luis Enrique anaonekana kuwa mstari wa mbele kabisa kuwa darajani msimu ujao. Maisha ni lazima yaendelee kwa sababu wanasema kuwa kocha are hired to be fired (makocha wanaajiliwa ili wafukuzwe).

Makala kama hizi pia unaweza kuziona katika page ya Football Events7910 facebook ,Account ya Ernest Mazengo pia facebook na ktk blog ya ernestmazengo.blogspot.com
Mawasiliano:+255 657 00 58 77 or +255 763 619 770 or +255 625 76 13 88
Email:ernestmazengo@gmail.com
Prepared By
Mr Mazengo {Football Pundit /Analyst}
Please share na washikaji…Thanks.
 
Tatizo la Conte ni uwezo mdogo wa uvumilivu na kusuluhisha migogoro ingali haijakua mikubwa ya wachezaji wanapofanya makosa.

Mgogoro wa Costa na Luis ndiyo inamuondoa,wachezaji siyo wajinga kiasi waone mwenzao anafanyiwa halafu wajitoe 100% japo si wote,yalimtokea morinho.
 
Mwenda mwana kwenda.
 
Na ndio kawaida ya kitu kinaitwa team mara nyingi ukimtendea mwenzao ubaya watakuuliza ndivyo wote tutakavyoyendewa ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…