TIMU ya soka ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, leo ina kibarua kigumu dhidi ya vijana wenzao wa Madagascar katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa yakiwa ni maandalizi yao kabla ya kuwavaa vijana wa Afrika Kusini kuwania kucheza fainali za Afrika zitakazofanyika jijini Antananarivo, Madagascar kati ya Aprili 2-16, 2017.
Serengeti Boys imepiga kambi jijini Antananarivo, Madagascar kujiandaa kucheza na Afrika Kusini katika mchezo mgumu wa awali kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Agosti 6, 2016.