LGE2024 Makalla: CHADEMA acheni visingizio, migogoro ya ndani ya chama chenu na maandalizi mabovu ni kisiki kwenu kufanikiwa Uchaguzi Serikali za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2020
Posts
2,823
Reaction score
2,466

Your browser is not able to display this video.

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA Amoss Makalla ameitaka Chadema kuacha visingizio vya kulalamikia wagombea wake bali iseme ukweli kuwa haikufanya maandalizi kuingia katika Uchaguzi wa serikali za mitaa.

Pia, amesema chama hicho kinazongwa na migogoro ambayo inakiweka pabaya kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu.

Akizungumza leo Novemba 25, 2024 katika Jimbo la Kinondoni Jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa mikutano yake ya kampeni ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, CPA Makalla amesema kuwa CHADEMA wamekuwa wakitumia kichaka cha wagombea wao kuenguliwa katika uchaguzi huo.

"Tumekuwa tukiwasikiliza wenzetu na wanapiga kelele nyingi sana kuwa wameenguliwa na wengine wanatumia kuenguliwa kama kichaka cha kuficha madhaifu wao.Ukweli ni kwamba CHADEMA hawakujiandaa kwasababu mbili, moja baada ya Rais DK.Samia Suluhu Hassan kuruhusu mikutano ya hadhara waliamua kuwekeza katika maandamano ya nchi.

SOMA PIA: Special Thread: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

"Wakati wanafanya maandamano CCM tulikwenda kwa wananchi kueleza kuwa mwaka huu kuna uchaguzi muhimu wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji pamoja na kutekeleza Ilani kwa ajili ya kuleta maendeleo ya wananchi,"amesema CPA Makalla.

Pia amesema CCM waliamua kutoa mafunzo kwa wagombea wake kupitia wanasheria kuhusu ujazaji wa fomu za wagombeq maana walitambua umuhimu wa kujaza fomu hizo kwa usahihi.

"CCM tuliandaa wagombea wetu kwa kutumia wanasherea kupata mafunzo ya kujaza fomu za wagombea. Wenzetu hawakujiandaa na ndio maana walipokuwa wanajaza fomu mtu anaambiwa jaza jina lako anajaza mwaka wa kuzaliwa , anaambiwa jaza mwaka wa kuzaliwa anajaza namba ya simu."

Alisisitiza "CHADEMA kwa sasa Wana mgororo mkubwa wa viongozi na ndio maana wameshindwa kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa na badala yake wamekuwa wakijificha katika kudai wameenguliwa".
 
Makalla anawachapa za uso kweli kweli ni huyu Mwenezi CCM ilimuhitaji kwa muda mrefu.
 
Mgogoro ndio uliowakata wagombea wao?
 
sema baba sema, wakuskie vizuri 🤣
 
Migogoro ndiyo imefanya muwaengue 70% ya wagombea wao? Huyu guluguja Makalla hovyo sana
 
Makalla ni chuma sana
 
Makalla ni balaaa
 
Nilikuwa ninamchukulia poa kumbe Makalla anajua siasa jamaa kaongea hoja nzuri na ni kweli Chadema wamekosa maandalizi mazuri na wanakosa mikakati madhubuti ya kushinda uchaguzi wa serikali mitaa badala yake wamejificha kwenye kuenguliwa ili wakishindwa iyonekane wamefanyiwa figisu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…