Minyukano ya makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), inayoendelea kupigania Jimbo la Kigamboni imeuibua uongozi wa Chama hicho unaodai haufurahishwi na vitendo hivyo huku ukiahidi kuwashughulikia iwapo hawata jirekebisha.
Chanzo cha vurugu hizo kushamiri katika eneo hilo ni baada ya aliyekuwa Mbunge wake Dk Faustine Ndugulie na aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, kufariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 27, 2024 nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amewakosoa baadhi ya Wanachama wa CCM wanaoonesha nia ya kuwania Jimbo la Kigamboni lililokuwa likiongozwa na marehemu Faustine Engelbert Ndugulile kinyume cha utaratibu.