LGE2024 Makalla: Msiwachague Wapinzani

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

CM 1774858

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
5,621
Reaction score
5,029


KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla amesema vyama vya upinzani haviaminiki, wala viongozi wao hawaaminiani, hivyo wagombea wake hawastahili kuchaguliwa.

Makala amesema hayo wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika Kata ya Manzese, Jimbo la Ubungo, jijini Dar es Salaam, leo tarehe 24 Novemba 2024.

CPA Makalla alitoa wito kwa wananchi kuwachagua wagombea wa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Makalla alisema vyama hivyo vya upinzani haviwezi kuaminiwa kupewa nafasi ya kuongoza mitaa, vijiji wala vitongoji, kwa sababu viongozi wake hawana uadilifu.

"Hela tu ya majimbo walikuwa wanatafuna hawa ndiyo uwape mitaa hiyo mihuri itakuwa salama?

"Hawaaminiki wa lolote na wao wenyewe hawajiamini. Mwaka 2020 walipata wabunge 19 wa viti maalum, lakini wakawatimua, mna uhakika gani hawa wenyeviti wakichaguliwa kama hawatawatimua?," alihoji CPA Makalla.

Alisisitiza: "Wabunge wao wakawapa jina baya COVID 19 lakini licha ya kuwapa jina baya lakini ruzuku wanachukua."
 
Ccm mmetuletea wananchi umaskini kwa miaka 60 tangu uhuru! Nyerere alituachia viwanda vingi nyie mmejiuzia. Karne hii bado tunazingumzia matundu ya choo,Kuna shule hazina madawati wengine wanasomea chini ya miembe. Ondokeni hatuwataki tena. Tunachagua hao wapinzani watatufaa sana
 
View attachment 3161492

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla amesema vyama vya upinzani haviaminiki, wala viongozi wao hawaaminiani, hivyo wagombea wake hawastahili kuchaguliwa...
Ccm mmetuletea wananchi umaskini kwa miaka 60 tangu uhuru! Nyerere alituachia viwanda vingi nyie mmejiuzia. Karne hii bado tunazingumzia matundu ya choo, kuna shule hazina madawati wengine wanasomea chini ya miembe. Ondokeni hatuwataki tena. Tunachagua hao wapinzani watatufaa sana
 
Nyerere alikuwa chama gani?
 
Nyerere alikuwa chama Gani?
 
 

Attachments

  • 5888170-bf4e11cfdbb5cf4f872954d4ae022fd6.mp4
    4.4 MB
Your browser is not able to display this video.
 
Wawachagueje sasa na mmewakata wote?

Si mngewaacha wapambane na hao ccm ili mseme hizi kauli?
 
Safi sana Pacha
 
Alisisitiza: "Wabunge wao wakawapa jina baya COVID 19 lakini licha ya kuwapa jina baya lakini ruzuku wanachukua."
Lahaula lakwata hii kesi nzito hii hapa sijaelewa vizuri yaan ndio kusemaje?
 
Makalla ni super sana huyu Mwenezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…