Pre GE2025 Makalla: Profesa Kitila Mkumbo ni hazina kubwa kwa Chama na Taifa

Pre GE2025 Makalla: Profesa Kitila Mkumbo ni hazina kubwa kwa Chama na Taifa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Posts
882
Reaction score
3,337
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, amemsifu Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo, kwa kujitoa kwa wananchi licha ya kuwa na majukumu makubwa ya kitaifa.

Pia soma > Prof. Kitila Mkumbo, mwanasiasa msomi ni somo jema kwa wasomi nchini

Akizungumza Jumatano, Machi 5, 2025, wakati wa kikao na viongozi wa CCM wa mashina, kata, matawi na mabalozi wa Wilaya ya Ubungo, mkoani Dar es Salaam, Makalla amesisitiza kuwa Prof. Kitila si kiongozi wa Jimbo la Ubungo pekee, bali ni rasilimali ya taifa nzima kutokana na mchango wake mkubwa serikalini na ndani ya chama. Amesema kuwa serikali na chama wanamtegemea kwa mipango ya maendeleo, hasa katika kuhakikisha dira ya maendeleo ya taifa inatekelezwa kwa ufanisi.

"Huyu mbunge wenu ni Waziri, lakini sisi kwenye chama tunamtumia sana. Ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ilani ya CCM, na pia ndiye anayeshughulikia Dira ya Taifa ya Maendeleo. Inaonyesha wazi kuwa anawapenda sana wananchi wake kwa sababu pamoja na ratiba yake ngumu, ameweza kufika hapa," amesema Makalla.

- Kitila Mkumbo: Boni Yai ni kama Mandonga kwenye ngumi, anaongea tu ila hana uwezo wa kunishinda.

 
Back
Top Bottom