Pre GE2025 Makalla: Uchaguzi Mkuu utafanyika kama ilivyopangwa, hakuna wa kuuzuia

Pre GE2025 Makalla: Uchaguzi Mkuu utafanyika kama ilivyopangwa, hakuna wa kuuzuia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema uchaguzi mkuu mwaka huu utafanyika kwa mujibu wa katiba na sheria kwani mabadiliko yameshafanyika, hivyo hakuna atakayezuia uchaguzi.

Makalla ameeleza hayo leo Machi 4, 2025 wakati akizungumza katika mkutano wa viongozi wa Chama na jumuiya ngazi ya shina, tawi, kata na wilaya katika Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es salaam, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano katika mkoa huo.
1741089684788.png
Soma, Pia
 
Ingekuwa jana hofu na uchaguzi kutofanyika wala asingekuwa na mda wakushughurka nalo ni kwa mfano TLP ndiyo ingetoa kauli ya CDM wala hakuna mtu angehangahika na hilo lakini CCM inajua kabisa CDm ina umati mkubwa wa watu nyuma yake zaidi yamilioni sita wanachama, washabiki pamoja na ndugu na jamaa zao ni pigo kama hao wote hawatajitokeza kupiga kura
 
Umwamba wa chama dola kongwe tawala CCM katika uchafuzi wa mchakato mzima wa kuelekea uchaguzi wa Oktoba 2025 unaweza kuwa na mazingira kama haya yanayotokea Uganda :

04 March 2025
Uchaguzi Kawempe North nchini Uganda, vyombo vya dola vyatumika

View: https://m.youtube.com/watch?v=cEGAwcuXDMc
 
Sasa wahusika wa huo uchaguzi ndio wanaotakiwa kusema hivyo labda wakili au Tume.
Sasa CCM mnawashwa na nini kulazimisha na kusisitiza uchaguzi upo au nyie ndio waandaaji wa huo uchaguzi.
Uchaguzi bila mabadiliko Hii kauli CCM imewaondoa kwenye reli.
 
Kwa maana nyingine chama hiki kongwe dola tawala CCM wanajivunia kutumia vyombo vya usalama vya dola ndiyo maana wana jeuri kama wenzao wa NRM huko Uganda wanatishia vyama vingine :

04 March 2025
Kawembe North, Uganda

Mkambiliano baina ya Vyombo vya Dola na Wapinzani

View: https://m.youtube.com/watch?v=WhkZcMp-OGA
 
Back
Top Bottom