Pre GE2025 Makalla: Wanaosema 'no reform no election' hawana fedha, CCM hilo halituhusu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amesema chama hicho kinaendelea kujipanga kwa uchaguzi ujao, huku akibeza kauli ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) inayosema hawatoingia kwenye uchaguzi pasipo kuwa na mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi.

Kamati kuu ya Chadema iliazimia kwamba 'No reform no election' uamuzi ambao umepigiliwa msumari na Mwenyekiti mpya wa Chadema, Tundu Lissu kwamba kwa sasa wanapigania mabadiliko ya sheria na si vinginevyo.

Leo Jumapili, Januari 26, 2025, akiwa Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar, Makalla amesema hao wanaosema 'no reform no election' hawana fedha wanatafuta sababu.
Your browser is not able to display this video.
 
Hizi ndo hoja za viongozi tunaowatumainia.
 

Ni kweli kabisa kwamba hakuna uwezekano wa kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu Mwaka huu wa 2025.
Aidha, ni kweli kabisa kwamba Hoja za Watu wa CHADEMA ni za kweli, pia ni za msingi. Hoja zao zina mashiko kuhusiana na Kukosekana kwa Mamlaka zinazoaminika kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi ulio huru, wa HAKI na ulio wa Wazi.

Jambo muhimu zaidi la kuzingatiwa ni kwamba: KAMWE CCM HAITAWEZA KUKUBALI KWA HIYARI KUBADILISHA MIFUMO YA UCHAGUZI. NA KAMWE CCM HAITAWEZA KUKUBALI KWA HIYARI KUBADILISHA KATIBA YA NCHI.

KAMWE HAUPO KABISA UWEZEKANO WA KUBADILISHA KATIBA YA NCHI KWA NJIA ZA KIDEMOKRASIA. HAUPO UWEZEKANO!

Kwa bahati mbaya sana, huu ndio Ukweli mchungu Sana kupita kiasi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…