Makamanda wa nhif wanaomba hongo!

Kenedy

Member
Joined
May 27, 2010
Posts
6
Reaction score
1
Ndugu wana jamii,
Leo nimeenda Regency kisha kumpeleka mtoto na mama. Kwakweli kunajaa kiasi kwamba hata madaktari wamejiwekea idadi ya watu wanaowahudumia. Tuliwahi kisha mimi nikapeleka kadi ya mtoto na mama ili kuwahi namba kama iivyokuwa siku zile za kuhesabu namba shule za msingi.
Nikatoa kadi ya mtoto na mama. Kuna kijana ambaye alisema ni afisa wa NHIF akasema mama yuko wapi. Nikasema, yuko nyuma anajikongoja anaumwa. Nikakataliwa katakata kupoandikisha jina la mama. Nikasema ni upuuzi kukataliwa kuchukua fomu kwa sababu mgonjwa kusimama dirishani siyo sahihi kama kuna aliyemleta. Nikadhani ni upuuzi tu huo, basi ngoja nimsubiri aje. Mtoto akaenda naye bahati mbaya alikuwa ameisha chelewa maana namba ilikuwa imeisha timia. Jamani mambo ya muhimbili yanatuumiza.
Nikaamua kurudi na kuchukua kadi ili nirudi nyumbani na tufanye mpango wa kuwahi kesho. Lakini nikanyimwa kadi ya mama. 'Kisa?' nikauliza, jawabu naambiwa nimetumia lugha ya chafu. Kwa hasira nikasema mara ya pili kuwa ni upuuzi na pengine ni kutokuwa na busara kumnyima mtu kadi yake anayelipia kila mwezi. Mke wangu akaenda akajikongoja mwenyewe kwenda pale dirishani, akapewa karatasi ya kuhudumiwa ila kadi nalazimishwa kuacha kazi zangu ili niende kuifuata kurasini ofisini kwao. Amemaliza matibabu amenyimwa kadi! Lazima amfuate huyu bwana ampigie magoti. Kisa utaratibu huu usiokuwa na huruma kwa wagonjwa. NHIF mnataka kujenga mlango gani huu?
Swali langu ni kuwa , adhabu ya kusema kuwa huu utaratibu wa kipuuzi ambao hata hauna hoja na kujua kuwa mgonjwa kusimama kwenye foleni si bora? Ninadhani haya mateso tumezoea na nadhani wanasheria wanaweza kunisaidia niwashitaki hawa wanadamu.
NHIF watafute mbinu njema ya kuratibu wanachama wao na siyo kuwataka wagonjwa wasimame dirishani, je kazi ya anayempeleka mgonjwa hospitali ni nini? Wanajamii tusaidiane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…