Makamba ahimiza mapambano dhidi ya ufisadi
na Jacob Ruvilo, Kigoma
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusufu Makamba, amesema ufisadi unapaswa kupigwa vita na kila Mtanzania mzalendo, kwani umechangia kwa kiasi kikubwa kudidimia maendeleo ya nchi.
Makamba alisema hayo juzi kwenye semina ya viongozi wa CCM Jimbo la Kigoma Mjini iliyofanyika katika viwanja vya Lake Tanganyika.
Alisema suala la watu kujipatia mali kinyume cha utaratibu na kuhujumu nchi havina uhusiano wowote na CCM, kwani watuhumiwa wote hawakuagizwa na chama kufanya hivyo, bali ni hulka zao binafsi.
Makamba alifafanua kuwa suala la muumini wa dhehebu fulani kwenda kinyume na maadili au amri ya vitabu vya dini, hapaswi kulaumiwa sheikh au mchungaji, badala yake ni muumini husika ambaye mwisho wa siku ndiye atakayepata adhabu kwa Mungu.
Aidha, Makamba alisema suala la vyama vya upinzani kushika bango na kuidhihaki CCM kuwa ni mafisadi kutokana na viongozi wachache wasio waaminifu, halina maana, bali suala la umoja na mshikamano katika kupinga mafisadi hao ni jukumu la watu wote, ikiwamo CCM.
Mbali na hilo, Makamba alikemea baadhi ya viongozi wa chama hicho kutumia uwezo wao wa fedha kutoa rushwa ili kupita katika chaguzi mbalimbali kuwa ni moja ya upatikana wa viongozi mafisadi na wasiofaa kwa jamii.
Alisema Tanzania haikuandaliwa kutawaliwa na wenye nacho na kwamba hali hiyo inaweka tabaka la mwenye nacho na a asiyenacho, hali ambayo isipoangaliwa kwa umakini suala la rushwa litabaki kuwa ndoto.
My Take:
Nasubiri kina Rostam na wenyewe waunge mkono vita hii!!