Makamba: Ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere umefikia asilimia 67

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
SASA ZIMEBAKI ASILIMIA 33 TU KUKAMILISHA BWAWA LA KUFUA UMEME LA NYERERE

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere umefikia asilimia 67 na kubaki asilimia 33 tu toka ujenzi huo uanze na kusema kazi iliyokuwa ikifanyika kwa miaka miwili na nusu, hivi sasa imefanyika ndani ya mwaka mmoja hadi kufikia asilimia hizo. Alisema Disemba 2018 hadi Juni 2021 mradi uliyoanza (miaka miwili na nusu) kazi ilifika asilimia 37, lakini kuanzia Juni 2021 hadi Julai mwaka huu, kazi imefanyika kwa asilimia 30.

Makamba alieleza hayo juzi mbele ya wajumbe wa bodi ya Tanesco, Wahariri na Wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari waliotembelea mradi huo kujionea hatua iliyofikiwa katika kipindi cha mwaka mmoja.

Katika ziara hiyo wahariri na wanahabari walipata fursa ya kujionea maeneo nane muhimu katika mradi huo ikiwemo:
Tuta kuu (main dam): ujenzi Juni 2021 ulikua 26%, sasa hivi 78%. 
> Daraja la kudumu (permanent bridge): Juni 2021 ulikuwa 37.8%, sasa hivi 95%.
Njia za maji kuendesha mitambo (power water ways ): Juni 2021 ulikuwa 43%, sasa hivi 85%.
Kituo cha kusafirishia umeme (switchyard): Juni 2021 kilikua 38%, sasa hivi 89.7%.

Akiongea kwa nianba ya wahariri na waandishi wa habari waliotembelea mradi huo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Nishati kwa hatua kubwa katika mradi huo. “Tulikuwa tunasikia tu mradi unaendelea lakini hatukuwa na taarifa sahihi. Tumeona, tunashukuru na tunapongeza hatua iliyofikiwa.” amesema Balile
IMG-20220810-WA0011.jpg
IMG-20220810-WA0012.jpg
IMG-20220810-WA0008.jpg
IMG-20220810-WA0010.jpg

PIA SOMA

TUHUMA ZA UFISADI NA HUJUMA

HISTORIA

Safi sana Makamba!
Haters sasa watafute uzushi mwingine maana ule wa 'hakuna chochote kinachoendelea' umeshakufilia mbali......napenda sana huu utendaji usio na mimbwembwe isiyo na msingi. Maana mbwembwe zikizidi basi hata wajinga, mashetani, wazushi, wenye wivu na wapuuzi hupata fursa ya kuongea na mwishowe matokeo ndo huwa kama vile ya uzushi uzushi tu.
 
SASA ZIMEBAKI ASILIMIA 33 TU KUKAMILISHA BWAWA LA KUFUA UMEME LA NYERERE

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere umefikia asilimia 67 na kubaki asilimia 33 tu toka ujenzi huo uanze na kusema kazi iliyokuwa ikifanyika kwa miaka miwili na nusu, hivi sasa imefanyika ndani ya mwaka mmoja hadi kufikia asilimia hizo. Alisema Disemba 2018 hadi Juni 2021 mradi uliyoanza (miaka miwili na nusu) kazi ilifika asilimia 37, lakini kuanzia Juni 2021 hadi Julai mwaka huu, kazi imefanyika kwa asilimia 30.

Makamba alieleza hayo juzi mbele ya wajumbe wa bodi ya Tanesco, Wahariri na Wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari waliotembelea mradi huo kujionea hatua iliyofikiwa katika kipindi cha mwaka mmoja.

Katika ziara hiyo wahariri na wanahabari walipata fursa ya kujionea maeneo nane muhimu katika mradi huo ikiwemo:

Akiongea kwa nianba ya wahariri na waandishi wa habari waliotembelea mradi huo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Nishati kwa hatua kubwa katika mradi huo. “Tulikuwa tunasikia tu mradi unaendelea lakini hatukuwa na taarifa sahihi. Tumeona, tunashukuru na tunapongeza hatua iliyofikiwa.” amesema Balile
View attachment 2320147View attachment 2320148View attachment 2320149View attachment 2320150
Daah
Ataje tarehe maana hizo asilimia hata kwenye keki Ipo
 
Waziri wa Nishati January Makamba amesema Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere litakamilika Mwezi June 2024.

Kwa sass ujenzi umefikia 67%

January alikuwa akijibu maswali ya wageni mbalimbali kwenye Sherehe za miaka 10 ya BBC Swahili

Source BBC Dira ya Dunia
 
Kila siku unamripoti makamba na hii taarifa ya asilimia 67 sio mara ya kwanza kuletwa hapa katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
 
Ovyo kabisa!Huyo jamaa kukosa nywele kumemfanya asiwe na akili hata kidogo leo Tanga cement wanapunguza uzalishaji kisa umeme hautoshi.Hivi mwekezaji gani atawekeza kwenye hii nchi?Kwa nini Mama alimuondoa Kalemani na kumleta huyo February?Mama alikosea na katukosea Watanzania Sana.
 
Enzi mradi huu ukijadiliwa Bungeni nakumbuka Halima Mdee alisemwa wazi kuwa kwa mradi huu kufanywa kwa miaka mitatu, ni uongo mkubwa!! Alishambuliwa kwa taarifa na miongozo ya akina Mlinga and co.

Mradi huu kwa sababu za kisiasa utatakiwa kutumiwa katika “tupeni nafasi tumalizie mradi mkubwa huu wa kimkakati” na wapiga kura walivo wasahaulifu, wataimba mapambio!!

June 2024, mradi hautakuwa zaidi ya 80%!!
 
Ovyo kabisa!Huyo jamaa kukosa nywele kumemfanya asiwe na akili hata kidogo leo Tanga cement wanapunguza uzalishaji kisa umeme hautoshi.Hivi mwekezaji gani atawekeza kwenye hii nchi?Kwa nini Mama alimuondoa Kalemani na kumleta huyo February?Mama alikosea na katukosea Watanzania Sana.
Mama alitaka kufanya kazi na vihiyo. Smart people watamu outsmart. Ndio maana kawaminya kina kassim na kina jaffo.
 
Waziri wa Nishati January Makamba amesema Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere litakamilika Mwezi June 2024.

Kwa sass ujenzi umefikia 67%

January alikuwa akijibu maswali ya wageni mbalimbali kwenye Sherehe za miaka 10 ya BBC Swahili

Source BBC Dira ya Dunia
Iko vizuri,kumbe mwaka 1 kabla ya uchaguzi..

Kujaza maji itachukua mda gani?
 
Back
Top Bottom