Makamba usipotoshe Nyanda za Juu Kusini hakuna ukame

Ameenda kupiga picha kwenye mito inayotiririsha maji kwa msimu halafu anatutangazia kuna ukame...

Jamaa sijui anatuanaje.

Si majuzi kati akaja na ile ya kusema watu walitishiwa wasifanye matengenezo kwa muda wa miaka mitano. Baada ya kuona hiyo kashtukiwa kaja na ya ukame. Sasa nayo wajuvi wamemkwida nayo. Sasa anabaki kusema mmh, mhm. Anabaki na kigugumizi.
 
Makamba anafahamika, ni mtandao wa msoga line, hayo yote anafanya ni mkakati wa kutuhujumu masikini
 
Huyu jamaa mshamba sana pamoja na kujifanya smart enough,kajikoroga sana toka ameingia hii wizara ,inabidi arudi kwa sangoma wake tena,ni full utapeli wa wazi mchana kweupee!
 
Mabwawa Yana Akina ya maji kujiendesha miezi sita hata Kama hakuna nvua kabisa,usitutie majaribuni tafadhari.
 
Kuna mstaafu anaogopa atakufa kama wenzake asumbua kutafuta pa kupiga kwa mara ya mwisho na sasa hivi atapiga pakubwa.Bundi wake yupo tanesco
 
Mabwawa Yana Akina ya maji kujiendesha miezi sita hata Kama hakuna nvua kabisa,usitutie majaribuni tafadhari.
Upo wapi wakati unaandika hizi pumba. Nenda ziara kuliko mabwawa na mito. Ukaja hapa hutakuwa unaandika kishabiki.
 
Hizo mvua za zinanyrsha kwenda angani. Acha kuwa wavivu wa fikra. Hayo maji mbona hapa mbarali hatuyaoni mito ikijaa.
Tukuyu kuna ukame we jamaa acha kuchekesha watu, Tukuyu ipi unayoisema.

Tofautisha kati ya ukame na uhaba wa mvua.
 
Mkuu sasa tukuamini wewe ama tumwamini Waziri - na kama anaendelea kuwa ofisini hadi muda huu maana yake Mamlaka yake ya uteuzi (Rais) imeridhika na utendaji wake wa kazi.
Kuwepo kwake ofisini hadi leo ni kwa sababu huenda Mamlaka yake ya uteuzi ina maslahi fulani na pia siyo vizuri kutengua kila wakati. Kumuonya na kumpa muda wa kujirekebisha kunaweza kufaa zaidi!
 
Kuna ukame nchi nzima. hata kule Tukuyu na Kitulo Njombe kuliko chanzo cha Great Ruaha hakuna mvua.
Mvua za huko nyanda za juu kusini, Mtwara, Ruvuma - zina anza week ya mwisho ya November! Sehemu hizo zina msimu mmoja (unimodal), tofauti na Dar, Pwani, Tanga, Kil, Arusha na lake zone zenye misimu miwili (OND - VULI) na (MAM - MASIKA) (bimodal).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…