Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
Nimemsikia Mwenyekiti wa NEC aliyeteuliwa na Mwenyekiti wa CCM kwenye wadhifa huo, Lewis Makame ktk Channel 10 leo usiku akisema tume yake haina uwezo wa kuwasaidia wanafunzi wa vyuo kupiga kura ktk sehemu za vyuo walikojiandikisha!! Kidogo niipasue TV yangu!!!!
Nikajiuliza: Hivi kweli NEC ni huru na taasisi inayosimamia demokrasia? Kwa nini tangu mwanzo alipoona vyuo vitakuwa bado vimefungwa asiahirishe uchaguzi kwa wiki moja tu ili wanafunzi wapate fursa ya kupiga kura? Kweli alikuwa hana uwezo huo? Au anafuata amri tu ya serikali ya chama tawala?