Kama kuna photo phobia
basi mie ninayo
napiga picha when necessary
Afu wanachoniudhi wapiga picha ni kukulazimisha kukupiga picha
tena ukimwambia hutaki ndo anakuwa kila saa anakuwinda.
huwa naboreka sana.
Misibani nako huwa nawaza
sijui hizo picha mtaziangalia lini
wakati mwingine unakuta na mwili unafotolewa kweli, dah!
I don't believe in picha Misibani.... Wakati tumefiwa na babangu (May he rest in peace) tuligoma kabisaaaa HATUTAKI Picha yoyote ile. Bahati mbaya ni kwamba unapokua kwenye majonzi huwezi anza bishana na wanaosimamia msiba badala ya kukalisha chini tokana na hali ya majonzi... Wakalazimisha na kuweka Mpiga picha na Camera Man ya the whole Process.. Tuliboreka mno!! Msiba ulipoisha tukaletewa Albam na Video... Walipo ondoka Mamangu akachukua albam na video akaanza kutazama, it did not take long akaanza upyaa kumlilia mumewe.... Baadae akavichukua na kuvitia mafuta na kuvichoma. Nyumbani tuna baadhi ya videos kuna babangu ndani... ana miaka saba chini sasa... Na hadi leo bado nakusanya guts za kuangalia zile video.... I still do not have the energy nahisi kufa nikifikiria kumuona na I can talk to him. Picha za Uhai wake I can stand... sio video...
HOWEVER.... Ni nzuri sometimes for ukiwa umefiwa huoni watu woote wanaofika pale, Mkanda waweza kupa picha halisi ya watu walofika pale. Ukiangalia waweza kua surprised wale ambao hukuwategemea walifika... Ingawa bado I am not conviced kua ina umuhimu wowote ule!
Pole sana AD.
Haina umuhimu aisee,labda kama unataka kulia for the rest of
your life,au kama una hamu ya kulia na hauna cha kukuliza ndo
utafute cd za msiba uangalie,sijui nani hua ana waleta watu kama
hawa msibani,hawajali hata ustaarabu.
Kama huyu aliye kuwa anachukua video leo,alikuwa anapokea simu mnaona kabisa
kwamba anaongea na simu (japo hamsikii) mbele yenu dah.
Kama kuna photo phobia
basi mie ninayo
napiga picha when necessary
Afu wanachoniudhi wapiga picha ni kukulazimisha kukupiga picha
tena ukimwambia hutaki ndo anakuwa kila saa anakuwinda.
huwa naboreka sana.
Misibani nako huwa nawaza
sijui hizo picha mtaziangalia lini
wakati mwingine unakuta na mwili unafotolewa kweli, dah!