Sina uhakika na sheria inayowabana, kuwaongoza ama kutokuwepo. Nina uhakika na jambo moja , nalo ni kuwa makampuni haya yanatoa ''rushwa ya kisayansi'' kuwaziba midomo waliopewa majukumu. Mfano, Unapomteua waziri mkuu mstaafu, au waziri kuwa mwenyekiti wa bodi maana yake ninini? Kampuni inapotoa ajira kwa watoto wa vigogo wenye ushawishi serikalini maana yake ni nini.? Tutarajie nini iwapo gavana wa benki mstaafu ndiye mwenyekiti wa bodi. Haiwezekani katika serikali yote hakuna asiyejua sheria, tatizo ni kwamba nani amfunge paka kengele endapo kuna makosa?
Hapa ndipo tunarudi kule kule yakuwa, tunahitaji katiba. Katiba itakayowapa viongozi uhuru wa kulitumikia taifa, kuwaongoz, kuwawajibisha na kuwahukumu ikibidi.
Hebu tujiulize ni sheria gani inayowapa haki ''western Union Tanzania'' kupokea fedha za kigeni na kuzibadilisha kwa viwango vyao, lakini sheria hiyo hiyo inawakataza kumruhusu mtanzania kutuma pesa nje? mbona kwingine duniani si hivyo? Je viongozi hawajui hili!!!