Hao vijana watafanikiwa kama wanaweza kuwa genuine maana movement ya wakosa ajira nchi yoyote huwa ina nguvu na inaweza kuangusha serikali.
Hao wataweza tu endapo wakihakikisha CCM haipandikizi mamluki wake humo wakawa wanapeleka taarifa za kimkakati , hii mbinu aliiweza Steven Ulimboka aliweza kuorganize na kupotea siku 3 ila movement ikawa inaendelea kuwa moto hata bila ya madaktari kujua yuko wapi hadi pale walipomtumia yule mhuni kupitia namba yake fulani ambayo ni watu wachache sana walikuwa nayo baada ya kutrace mawasiliano ya nyuma ndio wakamtesa na kumtupa msituni.
Hao vijana wakiweza kuchuja mapandikizi mission yao itafanikiwa kinyume na hapo watagawanywa kwa hongo na watasalitiana.