Makampuni yanayouza maji ya kunywa, pipi n.k wanapataje faida ukilinganisha na gharama za uzalishaji?

Tempus Fugit

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2016
Posts
850
Reaction score
2,212
Habari wadau...?
Niende moja kwa moja kwenye maudhui ya uzi huu. Huwa najiuliza sana kuhusu business plan ya makampuni yanayouza bidhaa kama pipi, au maji ya kunywa...

Wanatengenezaje faida ikiwa bei naona iko chini ukilinganisha na gharama zilizotumika kutengeneza bidhaa husika?

Mfano, maji ya masafi au afya au mengineyo, unakuta bei yake ni TZS 500, 700. Ila ukiangalia ile bidhaa imegharimu gharama kubwa za kiuzalishaji, kama vile kifungashio(chupa), imegharimu chemical process za filtration na purification, umeme, transport n.k

Au chukulia gharama zilizotumika kuitengeneza pipi moja mpaka imekuwa bidhaa inayoweza kutumika,..then pipi moja inauzwa TZS 50 au 100, au 200..

Halafu bidhaa moja kama maji inakuja kuuzwa 500 mtaani. Tena hiyo si bei ya kiwandani ambayo inakuwa chini zaidi..sasa kwa style hii haya makampuni yanapataje faida?

Maana mimi naona kama gharama za uzalishaji wa bidhaa hizo ni kubwa..na bei walau ingekuwa kubwa kidogo.

Kwa wenye kufahamu revenue model ya haya makampuni anitoe tongotongo.
 
Duh! Mkuu kiwanda kinatoa bidhaa kwa fungu moja kubwa na ndilo ukitoa kiwandani linakipa kiwanda faida hebu fikiria kreti moja la soda, fungu moja la maji ni shiling ngapi? Hapo ndipo kiwanda kinaangalia sio rejareja.
 
Ukitaka kujua yanavyopata faida, piga hesabu moja ya ndoo ya maji mtaani ya lita 20 ambayo ni kama shs 300. Uangalie wao wauza lita 1 shs 500. Pia kitaalamu gharama ya bidhaa za plastic zinaoimwa kwa kilo. Sasa kama kilo ya plastic ni shs 1000. Je kilo moja ya plastic inazalisha chupa ngapi? Utaona kuwa labda chpa ni senti 20 tu. Kwa ujumla gharama kubwa ni kodi na usambazaji. Vinginevyo faida ni kubwa tu. Ila pia maji yakubalike maana vimeanzishwa na kufa vingi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kuingezea faida wanaiona wanapouza labda lita 500,000 au 1m. Suala la vichupa chupa havijadiliwi kabisa kwenye production costs
 
Economy of scale faida kwenye hizi bidhaa ukitoa kila kitu inaweza ikawa hataTshs. 1/= kwa kila Unit..., ila kama kiwanda kinazalisha units 1,0000,000/= kwa siku, hio ni faida ya Tshs. 1,000,000/=, na kama faida ni Tshs. 10/= faida ni Tshs. 10,000,000/=

Its a Volumes, game Pile it High.., Sell it Cheap...,
 
Unatumika vigezo gani hadi unasema gharama ya kuzalisha chupa ya maji ya lita moja ni kubwa kuliko 500 au 700? Unahisi hayo makampuni hayana watalamu na wameamua kupata hasara? Waachie wenye mitaji yao wafanye biashara. Wewe ni mchanga katika elimu ya uzalishaji bidhaa.
 
Kwenye Biashara Tanzania bei iko kwenye mafungu haya
1. 50/
2.100/
3.200/
4.500/
6.1000/
7.2000/
8.5000/
9.10,000/

Model kama ya Cocacola wao wanatafuta sarafu, hawanashida na noti. Wanatafuta sh 500/
Pipi zote sijui maji wanatafita sarafu.

Mkuu Model ya kutafuta masarafu ndo the best model in the world.

KWA NINI?
Hizo bei ndo zile mtu anafanya consuption bila kulalamika au kujutia.

Mtu hawezi chenji Tsh 10,000 kununua pipi bali anatumia chenji chenji zilizo bakia.

Hizi bdo biashara zenye kuuza mno kwa sababu mteja hawazi mara mbilinbili.

Usha wahi kuona mtu anawaza kununua soda? Usha wahi mtu anajutia kununua pipi au karanga? Au maji?

Ni kwa sababu ametumia masarafu.

Kiwanda cha pipi chukulia wanazalisha pipi Milion 200 kwa mwaka.

Na faida ni sh 10. Maana yake watajuwa na faida ya bilion 2.

Au soda wanazalisha chupa milion 800 kwa mwaka nandaida yao ni sh 100 tu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo ndo product ambazo zinanunuliwa na masikini na tajiri bila mtu kulalamika.

Usha ona masikini anajutia kununua Pipi? Au soda? Cocacola inanunuliwa ba tajiri na masikini na wote wana ridhika.

Masikini na tajiri wananunua pipi na wote wanaridhika.

Hiyo model inalipa sana tena mno. Viwanda vya Soda wanauza sana si kwa sababy watu wanapenda soda no ni kwa sababu bei zao zinawezesha masikini na tajiri wote kununua.

SASA JE MASIKINI ANAWEZA NUNUA Iphone? Au Huawei? Jibu ni hapana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa maelezo mazuri
 
Ila bado ni biashara zenye changamoto kubwa kuliko zote.

Changamoto kubwa ni distribution na inventory management. Hapo ndio gharama za uendeshaji zinapokuwa.

Kitu cha 500 faida inapukutika mpaka unabaki na 50.

Ila Toyota anauza Landcruiser 1 kwa 250M. Wewe umeuza pipi au soda ngapi hapo hadi umfikie?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kijana unazngua unadhani kuna manufacturing companies zinajifanyia biashara tu bila cost accounting? Kuna wahasibu wanapiga costs of production za maji na izo pipi kisha wanaongezea % ya profit kwenye selling price ndio wanavyopata faida pia costs wanacalculate kwa batch ya ayo maji na pipi, we unaonekana hauna proffessionalism yoyote mana kwa mtu aliye na professionalism hawezi kuuliza swali kama ili
 
Asante mkuu kwa elimu hiyo. Lakini pia kwa opinion kuwa sina professionalism.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…