Makamu Mkuu wa Chuo hapa umenifunza

Hovering

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2018
Posts
275
Reaction score
912
Nikiwa chuo mwaka wa pili hii siku ilikuwa ni siku ya game ya UEFA (UCL knock out stage) kati Liverpool na team flani siikumbuki.

Kawaida yangu game kama hizi mara nyingi nilikua naangalizia 'Lounge' flani ambayo ipo ndani ya eneo la chuo na nafikiri Ile lounge ni mradi wa chuo.

Stuli ya wastani nimekaa counter, pembeni yangu watu wazima watatu na wawili kati yao ni wahadhiri 'lecturers' nawafahamu fresh. Kucheck game pale kiingilio ni kinywaji utakachonunua pale au huduma nyingine ya kulipia.

Natumia sana Sprite na pale kwa kipindi kile ni buku tu, hio hainishindi kabisa.

Hii game ilichezwa saa 4:45 usiku. Sasa dakika kama ya 15 hivi ya mchezo nashangaa wale 'lecturers' wanasimama kwa kufuatana wote wanamsalimia Mzee Moja wa makamo kwa nidhamu ya hali ya juu.

Kwa ule mkombo na ushapu wa tukio nikajikuta na Mimi nasimama huku macho yangu bado kwenye TV kisha kurejea kumuangalia huyu Mzee anayesalimiwa kwa nidhamu hivi ni nani. Asee! kumbe ni Vice chancellor wa Chuo. Kidogo nikaingiwa 'mteru' kiasi.

Mzee alikua 'casual' sana, mimi sikusalimiana nae 'in personal' zaidi ya heshima yangu ya mkumbo ya Kusimama tu.

Baada ya Salamu Mheshimiwa akatoa 'order' pale counter . "Kila mtu aongezewe kulingana na alichonacho. Kama ana bia mbili basi aongezewe mbili nyingine, kama ni maji ya Kilimanjaro apewe chupa nyingine".

Maanake Mimi mwenye Sprite niongezewe sprite ingine tena Moja tu. Wale wazee pembeni wakaendelea kuenjoy walikua wana shusha Mzinga mkubwa na vyupa kadhaa vya bia.
Sikujali sana kuhusu wale wahadhiri ila binafsi nilifurahishwa na 'offer' na ikafanya nifikirie mbali kidogo.

NINI NILIFIKIRIA

Kweli Bahati zipo, ila kama unataka uifahidi siku itakapokuangukia basi muda wote kuwa na maandalizi bora zaidi.

Vice chancellor kufika pale usiku ule tu kwangu ni bahati, maana si mtu unaweza kumfikia wakati wowote unaotaka wewe na akapatikana kwajili yako.

Inawezekana ni kawaida yake kuzuru pale majira kama yale Lakini kwangu sio kawaida. Ilitokea akanikuta na nikamuona bila changamoto yoyote hio ni bahati.

Lakini hili si kiini cha dhima yangu, maana yangu ipo kwenye tukio alilolifanya.

Turejee hapa "Kila mtu aongezewe kulingana na alichonacho. Kama ana bia mbili basi aongezewe mbili nyingine, kama ni maji ya Kilimanjaro apewe chupa nyingine". Hapa.

Niliongezewa Sprite yangu moja kwasababu nilikua na kunywa hio chupa moja. Yani ndio bajeti na maandalizi yangu yaliishia hapo.

Wale wahadhiri waliongezewa sawasawa na vinywaji vyao ambapo kwa kweli meza yao ilipendeza kwa jicho la kilevi.

Maana yake ni kwamba bahati ya ujio wa mkuu wachuo pale kwa wakati ule uliwaneemesha wao na Mimi pia japo kwa namna mbili zisizo lingana.

Hii sawa na kusema kwamba laiti kama ningekuwa napiga cocktail ya Grad malt na Coke baridi basi vingekuja kwa round nyingine. Ama lah! Juice ya box ya 3500 basi lingekuja box lingine.

Sasa tuiweke hii maana katika maisha ya kila siku.

Ni kweli wewe ni graduate, muajiriwa au mfanyabiashara mdogo, Je ukipata bahati Leo ya kupata kazi kwa wewe jobless graduate, au kupata chaka jipya kwa wewe muajiriwa, au mkopo wa riba nafuu wa mtaji kwa wewe mfanyabiashara respectively utanufaika pakubwa au padogo?
Jibu halisi unalo wewe.

Sasa huu muda wakati unasuburi bahati/ngekewa ukudondokee kwanini usiongeze thamani Yako.

Wakati Makamu mkuu wa chuo hajaja kwanini usiagize hata ubwabwa kuku makange kama bajeti inaruhusu? Utanielewa tu. Ngoja tuanze na Jobless.

Ndio bado unasoma au ni graduate lakini laptop yako kazi yake kubwa ni kuangalizia movies.

Kwanini usiongeze thamani yako kwa ku install na kujifunza software za kidigitali kama Adobe Premiere au Adobe Photoshop ujifunze kutengeneza matangazo madogo madogo ya kibiashara kwa njia picha au video. Hujawai kuwaza hiko huh!

Sawa ni Graduate, huu muda unaopiga mark time kwanini usifosi ufanye driving school walau upate hata leseni class D?

Bahati ikikudondokea itakuneemesha kulingana na thamani Yako kwa wakati huo. Ukiwa na degree yako umetulia na leseni Yako pembeni huoni umeongeza thamani.

Kazi za wenye degree sio tena level yako pekee, kazi za wenye degree na leseni ya udereva ndio eneo lako la kujidai na una fikiri hadhi yako itakua sawa na asiyekuwa nayo? , No!

Sawa ni graduate huna kazi, kwanini usipambane kuomba Scholarship za Masters ndani na nje ya nchi?.

Wakati huu ambao hujui ni lini utaajiriwa ukipata nafasi ya kuongeza thamani kitaaluma wapi unaingia hasara, hakuna.

Najua si rahisi hivo lakini onesha uthubutu kwanza. Bahati itakapokudondokea hutakuwa tena na thamani ya undergraduate bali ni post graduate.

Maslahi Vipi hapo huh? Imekaa poa hii!

Nakubali umeajiriwa japo usalama wa kazi Yako unajua wewe mwenyewe, ila hio WiFi ya ofisini kwanini usiitumie kuongeza thamani yako. Unajiuliza kivipi.

Badala ya kufatilia muendelezo wa tamthilia flani au udaku kwanini usijifunze lugha ya kigeni hata Moja (English, French, Italiano au Chinese) kupitia internet.

Ongezea thamani Yako mwenyewe. Vipi ukutane na fursa ya kada yako wamesisitiza Chinese language ni added advantage na wewe una basics zake ? Unajisikiaje hapo hio 'confidence'.

Namalizia na wafanyabiashara.

Wakati unasuburi upate huo mtaji au mkopo wenye riba nafuu wa kubust biashara yako kwanini hujatengeza hata logo ya kuvutia ya brand ya bidhaa au huduma Yako.

Buni mifumo inayoendana na teknolojia na utandawazi kwajili ya ku 'promote' biashara yako. Acha kutumia WhatsApp Business ku
jimaliza na magroup ya 'Biliani Nyama'.

Omba mtu tengeneza profile ya kibiashara kwenye WhatsApp Business ya simu Yako.
Instagram na Telegram vilevile.

Hizi ni mambo ambazo haziitaji pesa kufanya lakini pesa utakapo ipata itasaidia kuleta ufanisi mkubwa kuwafikia wateja kibao na pia ubora wa bidhaa zako.

To wind up.

Sio kwamba pesa hatuna au hatupati No, tunaweka pesa kwenye vipaumbele visivyo na faida zaidi. Kwa kudundiliza kidogo hichohicho ada ya driving school 150k-200k itapatikana tu.

Kila siku unapata buku ya kubuy bundle unashindwa kutenga 30k-50k kutengenezewa logo ya standard nzuri ya biashara yako. Si kweli.

Ukiweka vipaumbele kwenye mambo binafsi ya muhimu basi thamani Yako itapanda pia na sikumoja bahati ikikushukia utaneemeka pakubwa sawasawa na maandalizi Yako.

Mimi nasema Bahati Ipo!


Monetary doctor Southern Highland Lily Tony Thecoder
 
Andiko zuri mkuu... Mimi mwenyewe ni mfano mzuri wa hiki ulichokisema hapa
 
Mada kama hizi lazima ukute wachangiaji ni sisi vipanga ila wale wa uji wa bibi huwezi kuona hata nukta zao zaidi utaishia kuona wanaoview ni wengi kuliko wanaoandika .

Oukey noted mdogo wangu
Ahsante kiongozi, unachosema ni kweli. Wadau wa MMU😆
 
Karibu sana. Kuna Mdau anasema haoni uhalisia wa hiki Tz hii. Asee tuna kazi kubwa kubadili mitazamo .
Mkuu Mimi ni ushuhuda tosha tu juu ya ulichokisema hapo, nilivyomaliza chuo niliamua kujiongezea thamani ambayo pia ilinipa thamani😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…