Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar kimesema bila mabadiliko ya sheria na mifumo ya uchaguzi nchini, hakutakuwa na Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Said Mzee Miraji amesema hawatakubali kuwa na sheria mbovu za uchaguzi na haiwezekani wakurugenzi wa halmashauri ambao ni wateule wa rais kuwa ni sehemu ya maofisa wa Tume ya Uchaguzi.
Alisema hayo visiwani Zanzibar jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za chama hicho huko Rahaleo, mjini Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti huyo alisema wanapozungumzia mabadiliko ya sheria ili kuwapo wagombea huru kwa nafasi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na wabunge si jambo linalowanufaisha CHADEMA tu bali ni jambo litakalowanufaisha watanzania wote na wapenda demokrasia, hivyo wataendelea kusimamia hoja hiyo.
"Tunataka mgombea wa urais angalau apate asilimia 50 ya kura ndipo atangazwe kuwa mshindi. Haiwezekani mtu anapata chini ya kura ya asilimia 50 anatangazwa kuwa ndiye mshindi. Hii si haki, tunasema mtu huyo hajachaguliwa," alisema.
Miraji alisema wanataka mfumo wa uchaguzi uwezeshe watu wawili walioongoza kupata kura nyingi, uchaguzi urudiwe ili kupata mshindi stahiki.
Alisema wako tayari Uchaguzi Mkuu usogezwe mbele ili sheria ya uchaguzi ifanyiwe marekebisho na kuwa na uchaguzi huru na haki.