Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Katika mahojiano yake na mwandishi wa Habari Makamu Mwenyekiti NCCR Mageuzi, Joseph Selaasini amesema;
"Mpina aliliona hili, sababu alikuwa akipata upinzani wakati anaongelea suala hili bungeni, sio tu kutoka kwa spika bali hata kutoka kwa wabunge wenzake. Kwa maslahi ya nchi aliona alipeleke hili nje ya bunge sababu ni jambo ambalo linaathiri wananchi.
"Kwa maoni yangu, Spika asizuie jambo hilo, aache wananchi wajadili. Rais Samia ni mtu ambaye amejitabanaisha kukataa rushwa, haiwezekani yeye akatae rushwa halafu watekelezaji wa sera za nchi pamoja na ilani wazuie mambo kama haya yajadaliwe, watakuwa wanaenda kinyume na Rais mwenyewe. Kumuunga mkono Rais hamaniishi kuacha kuibua mianya rushwa, anayesimiama kokote kuibua mianya ya rushwa huyu anakuwa anamuunga mkono Rais. Spika asizuie watu wanaotaka kumsaidia Rais kupambana na rushwa.
"Mpina kama mbunge ana haki ya kuongea Watanzania pamoja na wapiga kura wake. Spika anatakiwa kusimamia jambo hilo kwa namna ambayo wananchi wataona haki ikitetendeka, yaani upande mwingine wapewe nafasi ya kutengeza hoja kinzani na zile alizotoa Ppina. Kumfungia Mpina wananchi wakakaa bila majibu maana yake ni kuwafanya wananchi wakubaliane na Mpina. Hoja haitatuliwi kwa rungu wala nyundo bali ni kwa hoja yenye nguvu zaidi.
"Spika ana haki ya kumpeleka mbunge yoyote katika kamati ya maadili, lakini katika hili mimi kama raia nadhani mahesabu yamepigwa vibaya. Kwa hatua aliyochukuwa maana yake watanzania watachukua upande wa mpina, kilichochokuwa kinatakiwa ni kufanya mjadala ili hoja za mpina ziuawe/kufutwa kwa hoja zenye nguvu zaidi.
"Kumpeleka kwenye kamati ya maadili wananchi wanaona anaonewa na hata mimi pia naona hivyo, sababu kwanini hoja zake hazijibiwi matokeo yake tunaingiza technicalities? Ndio maana hata mahakama iliondoa utaratibu huu, sababu ukishinda kwa technicalities lazima kutokee uonevu sababu unazuia upande mweingine usitoe ushahidi/usisikilizwe.
"Pamoja na Mpina kupelekwa kwenye kamati ya Maadili, tunachotaka Watanzania ni hii hoja ijadiliwe.
"Wito wangu ni kwamba; siingilii maamuzi ya Spika, lakini hoja ya Mpina ijadiliwe."
#KataaMachawa
#KataaUozo2025
====
Pia soma:
- Luhanga Mpina apewa siku 10 na Spika kuleta ushahidi wa Bashe kulidanganya Bunge
- FULL TEXT: Maelezo ya Ushahidi Wa Luhaga Mpina Kwa Spika Wa Bunge Dkt Tulia Ackson juu ya Waziri Hussein Bashe Kusema Uongo Bungeni kuhusu Sukari
- Spika Tulia amburuza Luhanga Mpina Kamati ya maadili