Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MAKAMU MWENYEKITI UWT TAIFA ZAINAB SHOMARI AKAGUA UJENZI WA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA ITIGI.
Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa, Zainab Shomari ameipongeza Serikali ya awamu ya 6 kwa kutekeleza Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Itigi iliyopo Kata ya Tambuka reli Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ambapo amesema Hospitali hiyo itakapokamilika itamaliza changamoto za Huduma za afya haswa ya akina mama na watoto.
“Rais Dkt. Samia ameendelea kuimarisha Huduma za Afya na hii si kwa hapa tu,Bali maeneo yote ya Tanzania ambayo tunapita kuna ujenzi wa hospitali lengo likiwa kumaliza changamoto za kiafya,hivyo wito wangu wasimamizi wa mradi huu muendelee kusimamia kwa uadilifu ili umalizike kwa wakati na kutumiwa kama inabyokusudiwa”amesema Zainab Shomari
Halmashauri ya Wilaya ya Itigi imepokea Jumla ya Shilingi Bilioni moja kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ambapo majengo yanayojengwa ni pamoja na Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD),Ujenzi wa jengo la Maabara,Ujenzi wa kichomea Taka na Ujenzi wa Jengo la wazazi.