Makamu Mwenyekiti UWT Taifa Atembelea Kituo cha Afya cha Kagongwa, Kahama

Makamu Mwenyekiti UWT Taifa Atembelea Kituo cha Afya cha Kagongwa, Kahama

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MAKAMU MWENYEKITI UWT MNEC. ZAINAB SHOMARI ATEMBELEA KITUO CHA AFYA KAGONGWA-KAHAMA

Makamu mwenyekiti wa UWT MNEC. Zainab Shomari mapema leo Agosti 28.2023 akiwa wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga ametembelea na kukagua kituo cha Afya cha Kagongwa Kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Kahama,ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Viongozi wa UWT Taifa inayoongozwa na Mwenyekiti wa UWT na Mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha cha Mapinduzi Ndg. Marry Chatanda kukagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025,pamoja na kuzungumza na wanawake wa Jumuiya ya Wanawake UWT na wana CCM.

Mradi huo umegharimu shilingi milioni 700,877,000 kwa ajili ya ujenzi wa Maabara,Jengo la mionzi,Jengo la wagonjwa wa nje(OPD),Jengo la wazazi,Jengo la kufulia nguo chumba cha Upasuaji,Vyoo vya wagonjwa,njia ya kupitia wagonjwa na Tanuru la kuchomea taka hatarishi.

Mama shomari amewapongeza wasimamizi wa mradi huo kwa kusimamia vizuri ujenzi ambapo kukamilika kwake kumesaidia kusogeza huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo.

“Azma ya serikali yetu ni kusogeza huduma muhimu za afya,hivyo kukamilika kwa kituo hichi kunarahisisha na kusogeza huduma muhimu kwa wananchi”amesema MNEC. Zainab Shomari

Viongozi wa UWT wapo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ambapo leo wanahitimisha Ziara yao ya Kikazi ya kuzungumza na wanawake wa UWT,wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla,kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025.

🗓28/8/2023 📍Kahama

UWT IMARA. JESHI LA MAMA. KAZI IENDELEE
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-08-29 at 11.57.28.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-29 at 11.57.28.jpeg
    62.2 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-08-29 at 11.57.28(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-29 at 11.57.28(1).jpeg
    59.4 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-08-29 at 11.57.29.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-29 at 11.57.29.jpeg
    67.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-29 at 11.57.30.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-29 at 11.57.30.jpeg
    42.9 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-29 at 11.57.30(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-29 at 11.57.30(1).jpeg
    58.5 KB · Views: 2
Back
Top Bottom