Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) bara, Stephen Wasira amesema Uchaguzi Mkuu ujao (2025) utafanyika kama utakavyopangwa na Tume Huru ya Uchaguzi nchini (INEC).
Wasira ametoa kauli hiyo alipokuwa akihutubia wafuasi wa chama hicho katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Jumanne Februari 11,2025 huku akitoa kauli hiyo kujibu kauli ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundi Lissu aliyedai Uchaguzi huo hautofanyika bila kufanyika alichokiita reform (maboresho) ya sheria.
Wasira katika hotuba yake amesema:
“Nataka niwaambie uchaguzi lazima utafanyika na wale waliosikika wanasema uchaguzi haufanyiki hadi reform, hiyo ni ndoto ya mchana, uchaguzi utafanyika na Watanzania wajiandae na CCM ijiandae kushinda kwa kishindo.”