Makamu Rais wa zamani wa FIFA afungwa miaka 9 kwa kula rushwa

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
MAREKANI: Makamu Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia(FIFA), Juan Angel Napout amehukumiwa kifungo cha miaka 9 jela baada ya kukutwa na hatia ya kosa la kupokea rushwa

Katika uchunguzi uliofanywa ndani ya chombo hicho kikubwa cha soka duniani, Juan alipatikana na hatia ya kuchukua mamilioni ya dola kwa njia ya rushwa

Hatua hii inakuja siku chache baada ya kifungo cha miaka minne alichopewa Mkuu wa zamani wa soka Brazil, Jose Maria Marin ambaye pia alihusishwa kwenye tuhuma hizo hizo

Wote kwa pamoja walikutwa na hatia ya kupokea rushwa kutoka kwa Kampuni kubwa ambazo zilikuwa zikijitangaza kupitia FIFA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…