Elections 2010 Makamu wa Rais awe NANI?

any body can be a vice president so long is hailing from tannzania island. this is not a big issue so long there are more than one million in isles he/she can be picked easily.

Yaleyale ya ku-simplify serious issues na kuzifanys sio big issued. Anybody anaweza kuwa vice-president maana yake nini? Watanzania wanahitaji kupata Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri Kiongozi, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa watakaoweza kuleta mbadiliko na kuiletea nchi yetu maendeleo. Tukisema it is not a big issue yoyote tu anaweza kuwa picked ni kutoitakia mema Tanzania. Hivi tutaendelea mpaka lini kuchagua watu maradi wanajitokeza kugombea uongozi badala ya kutafuta ama kuchagua watu makini wenye uwezo wa kuinyanya nchi hii na kuirejesha pale ilipostahili kuwa?

Kila siku watu wamekuwa wakirudiarudia kulitaja jina la Salim katika safu ya uongozi wa ngazi ya juu wa Taifa letu kwa sababu alionyesha uwezo mkubwa wa uongozi na angaliweza kuliongoza taifa hili kwa ufanisi mkubwa. Watu kama marehemu Mwalimu Nyerere , Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine wataendelea kutajwa hadi na vizazi vijavyo kwa sababu ya uongozi wao bora. Siamini kwamba watu kama hawa tunaowachagua kwa kuangalia sura zao ama kwa kuona kwamba it is not a big issue kuwachagua wataweza kukumbukwa na yoyote zaidi ya marafiki zao pale watakapomaliza uongozi wao. Ni pale tu watakapojirekebisha na kuiga yaliyokuwa yakiwaletea sifa viongozi niliowataja hapo ndio hukumu ya wananchi inaweza ikabadilika kwao na wakaweza kukumbukwa siku za usoni.
 
Salim is okay, but i'm not sure he will be compartible with JK's administration style.....and he showed that openly when he used Nyerere's forum to criticize him.
 

unauhakika Dr Salimu si fisadi??? Katika purukushani ya kuiua TTCL kwa kuanzisha CELTEL yeye hakuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL na kuna tetesi kuwa alikuwa na hisa CELTEL????
 
Katika kundi maarufu lililojulikana kwa jina la mtandao 2005 aliyebaki katika nafasi ya juu kabisa na ambaye bado sikio la Kikwete liko karibu naye ni Membe. Nadhani katika short list ya Kikwete jina la huyu halitakosekana labda kama Makamu ni lazima atoke Zenj. Na pia meshatajwa katika wale wanaofikiria kuingia kwenye kinyang'anyiro cha 2015.
 
unauhakika Dr Salimu si fisadi??? Katika purukushani ya kuiua TTCL kwa kuanzisha CELTEL yeye hakuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL na kuna tetesi kuwa alikuwa na hisa CELTEL????


what is tetesi, weka ushahidi....
 
Sioni umuhimu wa hiyo nafasi kumaliza kamatumbwi ketu...
Ifutwe tu kuna msululu wa makaimu Rais....
 
Kuna Tetesi kuwa Rais wa sasa wa Zanzibar anaitaka nafasi hiyo,na inaonekana kuwa Wakuu wa Nchi wanakubaliana nae!Lakini bado kuna mazungumzo ndani ya chama kuhusu nafasi hiyo nyeti,ambayo ni lazima Mteule atoke Zanzibar.
 
hapo kati ya waliotajwa hakuna hata mmoja atakayefit isipokuwa mpagani ngombale-mwiru! hana kashfa wala mtandao! tena ni mzee wetu mzoefu.
 
Balozi isac sepetu amesahauliwa this time?
 
Mbona mnashindwa kuelewa vitu vidogo tu? Sasa Prof. Tibaijuka ni mzawa wa visiwani?
 

Itakuwa vipi kipindi ambapo raisi wa Jamhuri atatoka, Zanzibar?
 
vp atakuwa seif khatib au shamhuna..hawa kwa muungwana ni wadau boraa tuu..

hata kimatendoo wanafanana naye sanaa tuu..wapenda michezoo hasa soka!!!! tehe tehe..

salim haiwezekani kwani amemzidii mno muungwanaa katika maeneo yote..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…