Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Mkuu Loth Hema unajipa matumaini hewa na inaonekana husemi Trends za kisiasa za Tanzania.

TZ ni zaidi ya uijuavyo
 
Nchimbi ni mpenda haki, asingeweza anaongoza huku raia wanateswa!
Mauaji yale hayawezi mpendeza mtu yeyote mwenye akili timamu.

Nje ya mada; Nchimbi ni kiongozi ambaye hapendeki sababu anapendda haki. Magufuli alimkimbiza kumficha kwenye ubalozi huko.
 
Kwa lugha nyepesi ni Rais mwenza.
 
Nchimbi hajachaguliwa na wananchi, alichaguliwa na ccm ndipo wananchi mkampigia kura kwa mgongo wa samia.

Mfano kipindi cha JPM, samia hakuchaguliwa na wananchi ila alipita kwa mgongo wa JPM
Hapana, si kweli, hii ni hoja ya kuungaunga.

Hoja ya laichagukiw ana CCM hata Samia alichagukiwa na CCM kama unataka kuamini hoja hii.

Hoja ya "wananchi wakampigia kura kw amgongo wa Samia" ni potofu. Samia na Nchimbi waligombania u Rais na u Makamu wa Rais pamoja, as a ticket. Kama unaongelea habari ya mgongo, wote wawiki waligombania nafasi zao kwa mgongo wa CCM.

Ukisema Nchimbi hajachaguliwa na wananchi kwa sababu uchaguzi uliharibiwa, nitakuelewa.

Lakini ukisema Nchimbi hajachaguliwa na wananchi kwa sababu hizi ukizotoa, naona unakatakata viuno tu. Huelewi dhana ya running mate. Huelewi dhana ya ticket.

Yani Tanzania mmempa rais nguvu hata ambazo hana kikatiba. Kwa kumuabudu tu.

Tukiondoa matatizo ya uchaguzi kutokuwa huru na haki na hivyo uchaguzi wote kuwa na doa, na tukichambua mfumo wa uchaguzi wa Tanzania in the abstract, kidhahania, Makamu wa Rais na Rais wanachaguliwa kwa kuwa kwenye ticket moja. Siku moja. Pamoja.

Kuna watu kibao washabiki wa Nchimbi wameichagua tiketi kwa sababu ya Nchimbi, wala si kwa sababu ya Samia.

Na hata kama uchaguzi ungekuwa wa huru na haki, hakuna njia ya kujua hao ni wangapi, kwa sababu mgombea urais na umakamu wa rais wanachaguliwa pamoja.

Sasa hapo utasemaje Nchimbi kachagukiwa kw amgongo wa Samia wakati kuna watu wameichagua hii tiketi kwa sababu ya Nchimbi, si kwa sababu ya Samia?

Kimsingi pale unapopiga kura humchagui Samia wala Nchimbi unawachagua wote. Kwa pamoja.

Hivyo ndivyo mfumo wa mgombea mwenza unavyofanya kazi. Ika Watanzania wengi hawajui hili.

IWatanzania wengi hawajui hilo, wanaona wanamchagua Rais, Makamu wa Rais ni sideshow tu.

Ndiyo maana Magufuli alivyofariki, watu waliooambiwa hatuhitaji kufanya uchaguzi tena, tulishamchagua Samia kama mgombea mwenza na Makamu wa Rais, huyu ndiye anakuwa Rais, waliona kama Samia anakuwa Rais bila uhalali.

Tanzania Rais anachaguliwa na Makamu kwa pamoja, as a ticket, mbona hamuelewi hili jambo jepesi tu?
 
aje asimame kwenye haki. wazanzibari wamewanyanyasa sana waTanganyika. kwenye katiba Mpya atapata nafasi kati ya zile KUU. Tundu Antiphas Lissu akiliongoza Taifa kwa weledi na mafanikio makubwa. wote tuseme Amina.
 
Majina matatu atawatajia Nape 😂
 
Kujiuzuru kwa Nchimbi CCM isione poa, freshi tu na kudai mbona Lowassa aliondoka na ikabaki na nguvu zake. Nguvu huwa zipo ila kuna wakati hutoweka ikadhani zipo na kujititimua kutunisha misuli kumbe ndio anguko lake. Nchimbi ni tofauti na Lowassa na nyakati ni tofauti.
 
zile damu zilizomwagika Oktoba 29, 2025 haziwezi kuiacha serikali haramu salama
 
Dunia nzima 98% tunaongoza sisi wanaume lakini still rushwa ufisadi, mauaji vipo itoshe kusema kiongozi bora hiahusiani na jinsia
 
Nchimbi na samia hawakugombea urais pamoja mana samia alipitishwa kihuni.

Sasa kama Nchimbi hajachaguliwa na wananchi kwa sababu ya uchaguzi kuharibika, inakuwaje samia awe amechaguliwa na rais?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…