Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Rais Samia alikuwa Makamu wa Rais na Majaliwa alikuwa Waziri Mkuu chini ya utawala wa Hayati Magufuli. Wakati huo mengi yalifanyika na hakuna siku wawili hawa waliwahi kupinga.
Baada ya Rais Samia kuingia amepingana kwa kiasi kikubwa na mtangulizi wake. Amepingana naye kuhusu uwepo wa mikutano ya adhara, amewarejesha kazini wale waliotumbuliwa kwa Kashafa nzito, amekiri uwepo wa COVID miaka ya nyuma nk.
Haya yote aliyofanya hakuna siku wakati wa Utawala wa Magufuli tuliwahi kusikia amepinga na hivyo kupelekea Magufuli kutenda kinyume na washauri wake.
Nikalinganisha JPM na Samia naamini wasaidizi wa Samia wamekaa kimya wakisubiri atoke madarakani wamkosoe. Matokeo yake badala ya kuendelea pale mtangulizi alipofika tunatumia muda mwingi kurekebisha mapungufu yake.
Je, kama Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wanashindwa kushauri vizuri kwanini wapo? Kama Rais ndiye kila kitu kwanini tunatumia gharama kubwa kumwekea Makamu na Waziri Mkuu?
Je, Rais Samia kuendelea na wasaidizi wanaosema yes kwenye kila jambo kuna afya kwa Taifa? Kuwa na wasaidizi ambao moyoni wanawaza tofauti na wanavyokushauri kuna tija?
Nadhani kama kuna Sehemu Rais Samia anakosea wasaidizi wake wamweleze sasa siyo kusubiri astaafu waanze kumkosoa kivitendo. Viongozi wakiwa wakweli na kukubali hata kujiuzulu pale ushauri wao unapokataliwa tutalisaidia sana Taifa letu.
Tumemwingiza chaka mama kwenye kikokotoo, mikopo ya asilimia 10, tumemshauri vibaya akawatumbua wasio na hatia tukijua , tumemshauri na kumpa taarifa za uongo kuhusu tozo, tumemdanganya kuhusu umuhimu wa Chawa kwenye maendeleo nk
Je, tunasubiri lini tumshauri ipasavyo? Tufanye sasa na Mwenyenzi Mungu atatubariki kwa vingi zaidi. Mama ni msikivu atatusikiliza tusiwe Chawa.