beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Shirikisho la soka duniani(FIFA) limempa kifungo hicho Makamu wa Rais wa Kwanza wa CAF, Kwesi Nyantakyi ambaye pia ni Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka nchini Ghana
Ni baada ya kubainika kupokea rushwa ya Dola za Kimarekani 65,000(Tsh. Milioni 148.85) kutoka kwa Mwanahabari aliyekuwa anafanya uchunguzi kuhusu ufisadi katika mchezo wa soka
Mbali na adhabu hiyo kali pia ametozwa faini ya Franc za Uswisi 500,000(takribani Tsh. Bilioni 1.135)
Nyantakyi, alijiuzulu mwezi Juni baada ya kuonekana kwenye ripoti ya uchunguzi iliyotolewa na Mwanahabari Anas Aremeyaw Anas, akipokea rushwa
Hata hivyo madai hayo aliyakanusha na kufuatia adhabu ya FIFA, haijafahamika iwapo atakata rufaa