Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Victoria Kwakwa, amesafiri kwa njia ya Treni ya Kisasa-SGR kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia.
Katika ziara hiyo, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), na Mawaziri wengine wa Kisekta kuhusu ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na uwezekano wa Benki hiyo kushiriki katika ufadhili wa vipande vya SGR vilivyosalia.
Bi Kwakwa alitumia fursa hiyo kuipongeza Tanzania kwa uwekezaji mkubwa wa mradi huo wa SGR ambao amesema utakuwa kichocheo kikubwa cha usafirishaji wa abiria na mizigo na kuchangia ukuaji wa uchumi si tu kwa Tanzania bali kwa nchi zote za Ukanda wa Maziwa Makuu.
Pamoja kushauri kuhusu umuhimu wa wananchi kuutunza mradi huo, Makamu huyo wa Rais wa Benki ya Dunia ameshauri suala la usafirishaji wa mizigo ya ndani na ile inayokwenda nje ya nchi ukaanza mapema iwezekanavyo ili kuchochea biashara na ukuaji wa uchumi utakaokuza ajira za watu.
Aidha, Kwakwa aliahidi kuwa Benki ya Dunia iko katika majadiliano na Tanzania namna ya kusaidia jitihada za Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kukamilisha mradi huo kwa ajili ya manufaa ya nchi na nchi jirani ambazo zitaungwa katika mradi huo ikiwemo nchi za DRC Congo na Burundi.
Katika safari hiyo Kwakwa aliambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Nathan Belete, na Maafisa Waandamizi wa Benki hiyo Nicholas Soikan na Makiko Watanabe.
Pia soma
~ NSSF inapanga kumpelekea Mahakamani Mkandarasi Mkuu wa Reli ya SGR, Yapi Merkezi
~ Wafanyakazi wa SGR (Lot 1) wafanya mgomo, washinikiza Mkandarasi awalipe stahiki zao ikiwemo NSSF
~ Mkandarasi wa SGR (Yapi Merkezi) anawaondoa Wafanyakazi kwa gia ya kuwapa likizo ya lazima, pia hajaingiza malipo ya NSSF
~ Yapi Merkezi: Hakuna Mfanyakazi wa SGR atakayefutwa kazi bila kulipwa stahiki zake ikiwemo NSSF