Kila mwaka ikifika desemba, tangia enzi za Moi, kule Kimalel wanakosema ndo kuna mbuzi wenye nyama tamu kabisa, huwa wanafanya 'auction'. Kimalel Goat auction. Wakulima wote huwa wanapeleka mbuzi wao mnandani afu wanauzwa kisha hela wanagawana wenyewe. Mwaka uliopita ilikuwa ni watu mashuhuri wanashindana kununua mbuzi. Afu ni lazima mbuzi wote mnadani wanunuliwe. Hapo usishangae kusikia kuna mbuzi aliyeuzwa kwa bei ya Kshs 100,000. Desemba njema sana kwa wakulima wa Kimalel, Baringo County.