Makange ya kuku

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
25,258
Reaction score
48,589
kitalembwa aliombaa hii

Kwanza muandae kuku wako au samaki vizuri mimi nilipata kuku wa kisasa nika mkata nusu kama hivi

Kwanza nilimuwekea viungo
Food color
Tangawizi ya kusagwa na chumvi

Nimamuacha kama lisaa hivi ili viungo vikolee nikaendelea na mambo mengine
Baada ya kulizika na mda na kuona kuki viungo vimekolea nikaanza kuweka mafuta kwenye sufuria baada ya kupata moto nikamuweka kuku wangu kumkaanga


Baada ya kuona kuku amekaangika vizuri

Baada ya hpo nikachukua vitunguu vyangu ambavyo nilivikata vizuri tu nikaweka

Vitunguu viziungue vilegee tu kama hivi usilazimieshe mpaka vibadilike rangi itakuwa mbaya

Nilipo lizika na uivaji wa kitunguu nikaamua kuweka hoho nilikata kwa style ya kusimama

Baada ya hpo nikaweka karoti

Ili ukate karot stlye hii lazima karot yako uilaze hivi na usiisimamishe

Baada ya hapo nikaweka nyanya kidogo tu wengine wana tumia tomato past mm siipend naon ina utamu utamu so nilisaga nyanya kidog tu moja tu niliisaga wengine hawaweki kabisa nyany ni wewe na mapenzi yako mimi nilipenda hivi

Nika koroga ili mchanganyiko uwe mzuri zaidi

Na makange yangu yangubyalikuwa hivyo kuku ni mtamu sana unaweza ukalia chips ndizi Half american napenda sana ndizi 😂 au ugali chakula chochote kile na mlo wakonukawa mzuri sana
 
WW ni ME au KE?
 
Hapa na NJAA sijala toka asubuh mpaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…