Makanisa mengi yametoka kwenye majukumu yao ya msingi

Makanisa mengi yametoka kwenye majukumu yao ya msingi

jerry13

Member
Joined
May 24, 2024
Posts
14
Reaction score
20
Habari wandugu,

Makanisa mengi ya kisasa yamekuwa yakiwapotosha waumini wao kwasababu kubwa ya kuacha majukumu yao ya msingi na kufanya majukumu yasiowahusu.

Jukumu la msingi la kanisa ni kuwasaidia waumini wao waboreshe mahusiano yao na Mungu kwa kutenda mema na kuacha mabaya.

Lakini siku hizi ukifuatilia mahubiri ya wachungaji, manabii, na mapasta wengi utaona mahubiri yao yamejikita kwenye mafanikio ya fedha, afya, mambo ya kurogana na kadhalika. Utasikia “pokea nyumba kwa jina la Yesu…Pokea gari kwa jina la Yesu”. Huu ni utapeli.

Makanisa yanabidi yarudi kwenye majukumu yao ya msingi wa kuhubiri neno la Mungu kwa kuwasihi waumini wao wamche Mungu kwa kutenda mema na kuepuka mabaya. Si ajabu uovu unazidi kukithiri kwenye jamii yetu; ubinafsi, ulevi wa kupindukia, uasherati, uchawi, ushoga na mambo mengine chungu mzima.
 
Back
Top Bottom