Makanisa ya ajabu ajabu yanashamiri kwasababu ya Tatizo la Afya ya Akili

Makanisa ya ajabu ajabu yanashamiri kwasababu ya Tatizo la Afya ya Akili

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Waziri Ummy amesema “Bila afya ya akili hakuna afya, lakini tunaogopa tunajificha katika kivuli cha unyanyapaa. Tutasikiliza kutoka kwa wachokoza mada tutaangalia tatizo la afya katika jamii, shuleni, afya ya akili kwa watoto, binafsi kama waziri nimeona tuvunje ukimya.”

Amesema tatizo la afya ya akili ni kubwa kwani sasa kuna wanawake wengi kwenye vipochi vyao wanatembea na maji ya baraka na mafuta ya upako.

“Lakini kushamiri kwa makanisa mengi ya ajabu ajabu ni changamoto ya afya ya akili,” alisema.

HABARI LEO
 
Huyu naye kaanza kuwa na matatizo ya afya ya akili. Mnajua fika kuwa kuna makanisa ya ajabu ajabu na hamyafungii mnaacha yaendelee na ninyi ni serikali mnakalia kubwabwaja tu.

Waziri jitadhimini yawezekana nawe una changamoto za afya ya akili.

#MaendeleoHayanaChama
 
Amesema tatizo la afya ya akili ni kubwa kwani sasa kuna wanawake wengi kwenye vipochi vyao wanatembea na maji ya baraka na mafuta ya upako.
Sasa yeye Ummy alitaka watembee na vilainishi kwenye Vipochi?

Aache kuingilia uhuru wa kuabudu.

Kuabudu sio Ugonjwa.
 
Ummy ambaye ni muislamu anajaribu kutukana mambo ya watu wa imani nyingine.

Mbona hajalalamikia baa zilizopo kila mahali na makelele usiku kucha?
 
Na kweli majitu mazima yanakubali ujinga eti kuna miujiza ya uponyaji. Mwambie hilo lichungaji liende Muhimbili, haliwezi kwenda maana linajua linawadanganya.
 
Back
Top Bottom