quito
Member
- Jul 20, 2013
- 69
- 43
Makao makuu ya mkoa mpya wa Rift Valley yatakuwa Kondoa. Mkoa huu ulipangwa kuanzishwa mwaka 2000 wakati wa utawala wa Rais Mtukufu Mh. Benjamin William Mkapa. Bahati mbaya waziri Mkuu wakati ule, Mh. Sumaye akapendekeza mkoa mwingine pembeni, karibu kabisa na mkoa wa Arusha zilikonyofolewa wilaya zote za mkoa mpya wa Manyara. Kwa wale wanaojua Jiografia wataelewa ninachokisema hapa. Mkoa wa Manyara hauko kimkakati (kisiasa, kijamii au kiuchumi), upo kwa sababu za mtu binafsi. Kwa mfano baadhi ya wilaya za mkoa wa Manyara zimepakana na mkoa wa Shinyanga (upande wa kaskazini Magharibi) wakati wilaya Kiteto inapakana na mkoa wa Tanga (kaskazini Mashariki) na Morogoro (kusini Mashariki). Uzuzu huu wa kimkakati ndio uliomfanya Sumaye aitwe Zero (Shinyanga, Morogoro na Tanga, wapi na wapi?). Inasemekana lengo lake ilikuwa apate nguvu za kisiasa za mkoa mpya dhidi ya Lowassa aliyekuwa na nguvu za kisiasa katika mkoa wa Arusha. Elimu yetu, kuanzia ya mkoloni hadi hii ya sasa ina makengeza. Sababu kubwa ni ukabila. Na hao wenye ukabila ndio wanaotuambia hakuna ukabila Tanzania. Angalia ramani ya mkoa wa Manyara (google) halafu niambie kama akili zetu siyo Zero basi ni Sifuri.