Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,443
- 4,006
Wakuu
Kama kichwa cha uzi kinavyosomeka, viongozi waandamizi na shughuli kadhaa zimesita hapo jijini Dodoma huku serikali ikitekeleza majukumu yake ya kazi nyingi kutokea huko jijini Dar Es Salaam wananchi hawaelewi mnawapeleka wapi na kwanini?
Kiongozi yeyote asiye fanya kazi kwa kuzingatia hisia na mahitaji halisi ya mwananchi anayemwongoza mwisho wake huwa majuto mjukuu.
Tazameni mlipoanguka, inukeni mrejee kwenye kushiriki anakotaka mwananchi kwenda kwa usalama wake na ninyi pia.
Vifuatavyo vimeligawa taifa kama ilivyo ujenzi wa tofali la chuma na udongo haliwezi kudumu kamwe kwa kuwa hakuna kiunganishi sahihi chenye kuleta vitu viwili hivyo kwa pamoja
1. Itikadi za kisiasa
2. Utawala na uongozi unaobadilika kwa kufuata mvumo wa ngoma ng'ambo ya mto
3. Chanjo ya UVIKO-19
4. Imani za kidini zisizosimamia uwepo wa Mungu aliye hai
5. Sheria zilizotungwa kutumika kama fimbo kukomoa kikwazo au kukwepa kujibu changamoto (Haki, Wajibu na Adhabu vinachonganishwa kwa sababu madhumuni yake ni matano kama kukatisha tamaa isitokee tena, kuondoa uwezo wa kutenda kosa, kukarabati tabia, kulipiza kisasi cha kutendwa isvyo halali kwa mjibu wa sheria, kurejesha mwenendo mwema ili amani na imani kutamalaki tena miongoni mwa waliotofautiana.
6. Wananchi wenye uchumi wa chini kukwepwa kuwezeshwa wakue na kufurahia nchi yao kwa amani na kujenga imani kwa uongozi na utawala
7. Kuthamini vya nje kuliko kuanzisha vya kwetu na kuongezea tu kwa maboresho kutoka nje
8. Kujengewa HOFU kiimani, kiuchumi, kiafya na kiusalama pasipo kujua udhaifu huo adui huutumia kama silaha ya kuingia na kuteka
Wenye mamlaka mnapewa RAI kuzingatia mwelekeo ulio chanya kwa wananchi msiwakatishe tamaa kutokana na maamuzi mnayofanya yakileta athari mnarejea kutoa ufafanuzi ambao huwa tayari umechelewa sana.
Mjumbe hauwawi