Makapuku Forum

Shindano kubwa la kusaka vipaji la Bongo Star Search ambalo mwaka huu linatimiza miaka 17 toka kuanzishwa kwake limetangaza kurudi kusaka vipaji kwenye Mkoa wa Kigoma ikiwa ni miaka 14 imepita toka lifanye msako kwenye Mkoa huo.

Hayo yamesemwa na Chief Judge Madame Rita ameyasema haya wakati akitangaza ratiba ya BSS 2023 ambapo Timu hiyo itakuwepo Kigoma October 28 na 29 baada ya kutoka Arusha watakakokuwa October 7 -8, Mwanza October 14-15, Mbeya October 21-22 na Dar es salaam November 3, 4 na 5.

@MsRitaPaulsen amesema vipaji, vitimbi na viroja vya msimu huu wa 14 vitakua vikioneshwa kwenye Chaneli ya STARTIMES SWAHILI kwenye kisimbuzi cha @startimestz kila siku za Jumapili saa tatu usiku na vionjo vitaoneshwa kila Jumatatu, Jumatano na Ijumaa ikiwa na kauli mbiu ya "Kipaji chako mtaji wako"
 
NMB Foundation leo imefungua rasmi dirisha la pili wa ufadhili wa masomo na usimamizi kwa mwaka 2023/24 kwa Wanafunzi wanaojiunga na Vyuo Vikuu kupitia Programu ya NMB Nuru Yangu Scholarship and Mentorship ambayo itafadhili Wanachuo 65 mwaka huu na 65 wa mwaka jana kwa kiasi cha Sh. Bilioni 1.

Ufadhili huo unatolewa kupitia Asasi ya Kiraia ya NMB Foundation iliyo chini ya Benki ya @nmbtanzania ambayo imejikita kusimamia na kufuatilia kwa karibu maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Sekta za Kilimo, Elimu, Afya, Mazingira na Ujasiriamali…. kwa mwaka jana pekee ilifadhili Wanafunzi 65 ambao hadi sasa wanaendelea na masomo katika vyuo vikuu mbalimbali.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa dirisha la maombi linaloanza Septemba 15 hadi Oktoba 8, 2023, Meneja Mkuu wa NMB Foundation, Nelson Karumuna alitaja sifa za Waombaji kuwa ni ufaulu wa kidato cha sita wa daraja la kwanza pointi 3 hadi daraja la kwanza pointi 7, pia kwa Wanafunzi wenye mazingira magumu na wenye changamoto.

“Ufadhili huu ambao unaenda katika maeneo ya ada, nauli, posho, stationary, mafunzo ‘field’ na laptop, unatolewa kwa Wanafunzi wanaojiunga chuo katika fani za hesabu na takwimu, biashara, uchumi, teknolojia, habari na mawasiliano, uhasibu, uhandisi, mafuta na gesi, sayansi pamoja na udaktari"

“Mwaka huu tutafadhili wanafunzi 65, hivyo kuifanya NMB Foundation kuwa na wanafunzi 130 hadi Mwaka wa Masomo wa 2023/24 utakapoanza, tunawahamasisha Watanzania wote kufikisha taarifa hizi kwa Wanafunzi waliomaliza ‘form six’ mwaka huu ambao wanajiandaa kujiunga Vyuo vikuu, kutembelea tovuti yetu ya www.foundation.nmbbank.co.tz wajaze fomu kwa usahihi ili kuepuka makosa yanayoweza kuwatoa kwenye mchakato wasomi wenye vigezo,” alisema Karumuna.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya NMB Foundation, Bi. Ruth Zaipuna, aliweka msisitizo kauli ya Meneja Mkuu wake akiwataka waombaji wahakikishe wanajaza fomu zao kwa usahihi, ili kuepuka makosa kama yaliyochangia kutopata Wanafunzi 100 waliowahitaji mwaka jana badala yake wakapata 65 tu.
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Wakazi wa Mikoa ya Kusini ya Mtwara, Lindi na Ruvuma hawatokuwa wanasafiri tena kwenda Dar es salaam kufuata huduma za matibabu kwakuwa huduma zote zitapatikana Hospitali mpya ya Kanda ya Kusini ikiwemo huduma ya kusafisha figo na mionzi ya Kansa.

Akiongea na Wakazi wa Mtwara katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona leo, Rais Samia amesema “Asubuhi nimekwenda kuona Hospitali ya Kanda ya Kusini iliyojengwa hapa Mtwara ni Hospitali ya Kisasa ambayo itahudumia Mikoa mitatu ya Lindi, Mtwara na Ruvuma ni Hospitali ya magonjwa makubwa Watu wakishindikana huko Hospitali za Mikoa watakuwa wanakwenda pale”

“Lililonifurahisha zaidi ni huduma mbili ambazo zamani tulikuwa tunapata Hospitali za Kitaifa pekee yake, huduma ya kusafisha figo sasa itafanyika hapa Mtwara vifaa vimeshafika nimeviona mwenyewe bado kufungwa kwahiyo wote watakaokuwa na matatizo ya figo tiba itafanyika hapa”

“Utafanywa pia upasuaji wa mifupa, moyo na huduma nyingine za Kitaifa, huduma ya mionzi kwa wanaogua Kansa pia zitatolewa kwenye Hospitali ya Kanda ya Kusini, kwahiyo hakuna sababu kwa Watu wa Mtwara, Lindi na Mtwara kuja Dar es salaam, huduma zote zitatolewa pale”

“Nimeambiwa eneo ni kubwa sana, nikanong’ona na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu nikamwambia lazima mlete kiwanda hapa kitakachokuwa kinazalisha yale maji wanayotiwa Wagonjwa badala ya kutegemea kusafirishwa sasa kiwanda kile kizalishe maji pale”
 
Bungwa wa malooser ka mpiga bingwa wa mabingwa
 
[emoji599] STRAIKA wa zamani wa Simba na Yanga aliyetupiwa virago vyake msimu huu na Singida Big Stars aliyoipandisha Ligi Kuu na kuichezea msimu uliopita, Amissi Tambwe amesema ameuandikia barua uongozi wa klabu hiyo akiupa siku saba ili ukamalishe madai yake kabla hajatimkia Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) kushtaki

“Bado nina mkataba wa mwaka mmoja na Singida, ila wamenisitishia bila ya mazungumzo na cha kushangaza nalipwa mshahara wangu kila mwezi, lakini madai yangu ya fedha za usajili hayafanyiwi kazi,”

“Nimeongea na Mwanasheria wangu ameniambia tayari amewatumia barua kuwaamuru wanilipe fedha yangu ndani ya siku saba tangu aitume barua hiyo na kama watashindwa kufanya hivyo mpango wangu ni kwenda FIFA,”
 
PART 2: Tambwe amefunguka kuwa baada ya msimu uliopita kumalizika alirudi kwao Burundi kwa mapumziko na muda wa kurudi ulipowadia ili kujiandaa na msimu mpya alizungumza na uongozi juu ya kutumiwa tiketi ya ndege lakini walikuwa wakimuahidi bila utekelezaji, kabla ya kuambiwa hatakuwa tena na timu hiyo.

“Sikutumiwa tiketi, ila baadaye tulifanya mazungumzo na nikaambiwa hawatakuwa nami kikosini kwa msimu huu bila sababu yoyote na kukubaliana kunipa madai yangu, lakini hadi sasa hawajafanya hivyo na wamekuwa wakiniingizia mshahara kama kawaida,”

“Shida yangu ni kulipwa fedha yangu ya usajili ya msimu mmoja uliobaki ambao naingiziwa mshahara kama makubaliano yetu yalivyokwenda shida ni fedha ya usajili ambayo taarifa yake ipo kwa mwanasheria wangu na ameifanyia kazi kwa kuutaka uongozi kunilipa kama makubaliano yetu yalivyokuwa,”
 
CAF CHAMPIONS LEAGUE
.
[emoji1232] AL MERREIKH Vs YANGA SC [emoji1241]
[emoji354] 16:00
[emoji2522] Pele Stadium
.
Yanga ina wachezaji bora ndani na nje ya uwanja hawa ndio waliofikisha kwenye fainali ya Shirikisho msimu 2022/2023. Imemuuza Fiston Mayele lakini wamefaidika na maingizo ya wachezaji wapya ambao wameongeza
ubora wa kikosi na kubadilisha kabisa hata staili ya uchezaji.

Al Merrekkh wamebomoka sana hasa baada ya kutokea machafuko nchini mwao na kuwafanya baadhi ya wachezaji wake muhimu kuondoka na imekosa mechi za kiushindani pamoja na mzuka kama walionao Yanga. Kila la kheri @yangasc [emoji1241]
 
Madereva wa malori ya mizigo katika mpaka wa Tunduma, mkoani Songwe wamelalamika kukaa zaidi ya siku kumi mpaka wa Tunduma wakisubiri kuvuka kwenda Zambia.

Madereva walitoa malalamiko hayo katika kikao chao na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dk Francis Michael aliyekutana nao kusikiliza changamoto wanazopitia.

Mmoja wa madereva Peter George, amesema yupo hapo mpakani kwa siku ya 12 sasa, huku akieleza kuna hujuma zinazofanywa na watumishi kupitisha magari madogo yakiwa yamebeba mizigo kwa kuyasindikiza huku wakiwaacha wenye malori kwenye foleni.

“Mimi nipo pale kichangani, inapofika saa sita kwenda saa saba, utaona kuna gari inakuja inashuka ikiwa na mzigo mzito, huku gari za tenki za mafuta zikifuata nyuma, watu wamechoka,” amesema George.

Halfani Hlahan amesema Kasumuli ni mpaka mdogo lakini unapofika pale unachukua karatasi unamkabidhi wakala anapeleka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), unaingia upande wa Malawi nako unakaa saa tatu hadi nne unaondoka.

“Kwa nini hilo hapa Tunduma linashindikana, kuna mzizi gani, gari lenye mafuta linakaa siku tano na nyaraka zimetoka?.” alihoji dereva huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa, Dk Francis Michael amesema serikali imeliona tatizo hilo, na mkandarasai anayetakiwa kujenga barabara nne katika eneo hilo ameshafika ofisini kwake tayari kuanza kazi ambapo kukamilika kwake kutasaidia kuondoa tatizo hilo.
 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete @ridhiwani_kikwete amewatahadharisha Watumishi wa Umma kujiepusha na mikopo yenye riba kubwa maarufu kwa jina la "Kausha Damu" huku akisisitiza kuwa mikopo ya aina hiyo imekuwa ikidhalilisha na kutweza utu wa Watumishi katika Jamii.

Kikwete ametoa tahadhari hiyo wakati akiongea na Watumishi wa Halmashauri ya Busega Mkoani Simiyu wakati akihitimisha ziara yake Mkoani humo ambapo amesema mikopo hiyo imewafanya baadhi ya Watumishi kuathirika kisaikolojia na kushindwa kufika katika vituo vya kazi na hivyo kuathiri utoaji wa huduma bora kwa Wananchi.

Ridhiwani amesema mikopo hiyo ambayo huchukuliwa kwenye Taasisi za Kifedha zisizotambulika imekuwa na riba kubwa ambayo huwapelekea Watumishi kushindwa kuwasilisha marejesho na kupelekea kuuzwa kwa nyumba au vitu vya thamani wanavyovimiliki hivyo amewataka Watumishi kuanza kutumia Mfumo mpya wa kieletroniki wa kukopa (e-loans) ulioanza kutumika kuanzia Sept 1, 2023 ambao unamuwezesha Mtumishi kuomba mkopo pasipo kufika kwenye Taasisi ya Kifedha au Tawi la Benki.

Amesema mfumo huo umeanzishwa na Ofisi ya Rais - UTUMISHI na Utawala Bora ili kumsaidia Mtumishi wa Umma kupata mikopo katika Taasisi za Kifedha zinazotambulika na Mwajiri ili kumuepusha Mtumishi kukopa sehemu ambazo humpeleka Mtumishi kunyang'anywa kadi ya Benki.
 
Robert Lucas Mkazi wa Mtaa wa Ipogoro E Kata ya Ruaha Mkoani Iringa amekutwa amejinyonga chumbani na waya ya umeme kwa kujitundika katika paa la nyumba huku akiacha ujumbe uliosema ameamua kufanya hivyo kwasababu ya hila tu na asilaumiwe Mtu yoyote.

Pracilia Medard ni Mke wa Robert ambapo ameiambia @AyoTV_ kuwa yeye na Mumewe hawakuwa na ugomvi wowote na alikuwa haoneshi kama alikuwa Mtu mwenye huzuni bali alikuwa anaona Mume wake yuko sawa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Allan Bukumbi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema marehemu aliacha ujumbe unaosomeka “Mimi Robert Lucas nimezaliwa tarehe 29 /9/ 1975 nimeamua kufanya hivi kwasababu ya hila naomba Mke wangu msimsumbue wala Watoto wangu ninaoishi nao na kabla ya mazishi yangu naomba Mdogo wangu Rematus Lucas afike ndio nizikwe “

Mwenyekiti wa Ipogolo E amesema Robert alikuwa na Mtoto ambaye alikuwa anafaya mitihani ya darasa la 7 na Mtot huyo amechukuliwa na Mwalimu wake ili amliwaze huku akisubiri mazishi ya Baba yake.
 
Kwa mara ya kwanza nimemtazama kipa mpya wa Simba, Ayoub dhidi ya Dynamos. Simba wamelamba dume. Pamoja na kufungwa nyavu zake, lakini unaona sifa zote za kipa bora ndani yake.

Uwezo wa kuongea na mabeki wake ni wa hali ya juu. Ugawaji wa mipira ni levo nyingine. Hana papara langoni, miguu yake ni ufundi mtupu. Ayoub Lakred ni fundi kwelikweli. Hapa Simba wamepata mtu ambaye Aishi Manula anapokosekana kuna mtu wa kuziba pengo lake.

Bado Manula atabaki kuwa kipa bora kuzalishwa nchini miaka 10 ya hivi karibuni, lakini Simba wanaonekana watakuwa imara pale anapokosekana.

Aishi ni kipa aliyepitia mikikimikiki mingi ya nje na ndani ya uwanja. Ni ngumu sana kumpeleka benchi kirahisi, lakini Ayoub anajua. Huyu Mmorocco anajua sana mpira na Simba wamefanya uamuzi mzuri kumsajili.

Kufungwa kwenye mpira sio uwezo tu wa kipa, ni uwajibikaji wa kila idara. Sina lawama yotote kwake. Ni suala la muda tu. Atakuja kuimbwa muda sio mrefu. Najua na wewe unalipata nafasi ya kutazama mechi hebu niambie namna ulivyomtazama kipa mpya wa Simba, Ayoub. [emoji116]
 
Yanga iliuvunja mfupa ilioushindwa kwa muda mrefu kwa kuifunga Al Merrikh ya Sudan kwa mabao 2-0, huku wakiupiga MPIRA MWINGI kwenye Uwanja wa Kigali Pele.

Yanga ilipata ushindi huo ambao ni REKODI kwa klabu hiyo, kwani ilikuwa haijawahi kupata ushindi mbele ya wapinzani wao hao kwenye michuano ya CAF tangu mwaka 1978.

Katika mchezo wa jana Yanga ilitengeneza nafasi nyingi ambazo kama ingezitumia ingepata mabao mengi zaidi, hivyo mechi ijayo ni lazima iwe makini kwa vile Al Merrikh itakuja Dar ikiwa haina cha kupoteza kutokana na matokeo ya nyumbani.
 
Kama kuna kitu ambacho Simba ilipatia ni uamuzi mzuri wa uteuzi wa kikosi cha kwanza uliofanywa na Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’. kocha huyo alipatia kila kitu. Moses Phiri ni Mzambia. Mpinzani alikuwa Mzambia.

Phiri ni moja kati ya washambuliaji wenye kila kitu. Kumuanzisha ulikuwa uamuzi sahihi, lakini dakika 45 za kwanza ni kama alikuwa mtalii uwanjani. Hakukuwa na presha kubwa kutoka kwake kwenda kwa mabeki wa Dynamos.

Ni kama dakika 45 zote alikuwa anarukaruka tu uwanjani. Washambuliaji wana faida moja tu kubwa. Anaweza kucheza ujinga kipindi cha kwanza, lakini akafunga kipindi cha pili na kuwafuta machozi mashabiki. Mchezaji kama Phiri alipaswa kufanya makubwa kipindi cha kwanza.

Kelele zimekuwa nyingi sana juu yake. Mashabiki wengi wa Simba wanadhani kocha huwa anambania kwa kumuweka benchi. Wengi wanaamini ana uwezo mkubwa. Ana uwezo wa kuibeba Simba. Mechi kama hizi mara zote ndizo ni za kutengeneza heshima. Mechi za kutengeneza imani kwa kocha na mashabiki. Simba na Yanga huwa hazina uvumilivu wa muda mrefu. Ni aina ya timu zinazotaka matokeo chanya mapema.

Kwa dakika 45 za kwanza, kiukweli Moses Phiri amewaangusha Msimbazi. Alikuwa anarukaruka tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…