Makapuku Forum

Unanikosea adabu ujue.. Ina maana mimi ni mpuliza moshi, yani mtu kama mimi niwe navuta yale madude natoa moshi kama treni ya mwaka 47!!? [emoji23][emoji1787]

Shunie Makiwendo nyie mnaamini hili suala, mie natumia vitu haramu hivyo.. [emoji848]
Akisema baby wako sisi ni nani tusiamini watu wanatumia shuka moja maka akee [emoji1787]
 
[emoji1787] Mvumilie tu my wiii
 
Kamishna wa Kinga na Tiba kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Dkt. Peter Mfisi amesema Nchi zilizohalalisha bangi zina utaratibu thabiti ikiwemo kulima bangi hizo kwenye maeneo maalum na kuna kiwango kinachotakiwa ambapo amesema bangi ya Tanzania inayolimwa kwenye mashamba yasiyo rasmi kiholela haifai na haiwezi kukubalika kwenye masoko halali ya nje ya Nchi.

Amesema hayo leo Jijini Dar es salaam baada ya Mwandishi wa @AyoTV_ kumuuliza mtazamo wake kuhusu maoni ya Watu wakiwemo Wabunge kwamba bangi ianze kuuzwa nje ya Nchi ili iongeze pato la Taifa badala ya kuwa inateketezwa.

“Nchi zilizohalalisha bangi wana bangi yao inalimwa kwenye green house inatakiwa iwe na kiwango fulani, tusichukulie tu jambo la rahisi tu kwamba tutachukua tuweke kwenye kiroba kwenda kuwauzuia nje mfano Kenya, Kenya wenyewe bangi haijahalalishwa”

“Hii bangi yetu haifai kwenye kwenye masoko halali hata huko nje, kule wenzetu wametengeneza sehemu maalum za kuuza, kiwango cha kununua na hata umri wa Mtu wa kumuuzia, ukisema uruhusu ya kwetu haiwezi kukubalika, mfano halisi ni miwa, hivi miwa yote inaruhusiwa kutengenezea sukari?, jibu ni hapana, na bangi pia ipo hivyo sio kila bangi inafaa kwa matumizi halali”
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohamedi Mchengerwa amekiri kwamba walioshauri ujenzi wa mradi eneo la Jangwani ikiwemo daraja na miundombinu mingine kwa namna ilivyo sasa waliikosea Serikali lakini amesema wanakiri makosa huku wakijisahihisha na kwamba sasa Serikali ya awamu ya sita tayari imesaini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo ambapo ujenzi unatarajiwa kuanza mapema iwezekanavyo.

“Lazima tukiri kwamba waliotushauri tuijenge Jangwani kwa namna ilivyo sasa walitukosea lakini tukiri makosa huku tukijisahihisha,
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu tayari imesaini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo ambapo ujenzi unatarajiwa kuanza mapema iwezekanavyo”

Amesema hayo wakati wa ziara ya pamoja aliwa na Mawaziri wa Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Fedha ambapo wametembelea eneo la Jangwani ambalo limeathirika na mvua zinazoendelea kunyesha baada ya Mto Msimbazi kujaa ambapo amesema mradi wa uboreshaji wa Mto Msimbazi unaotegemewa kuanza hivi karibuni utatatua changamoto za miaka 100 ijayo na sio baada ya miaka 10 tena kuwe na changamoto kama za sasa .

Amesema tayari Serikali kupitia OR-TAMISEMI imesaini mkataba wa kupata fedha kutoka Benki ya Dunia zitakazo wezesha kutekeleza mradi mkubwa wa uboreshaji wa Bonde la Mto Msimbazi ikiwa ni pamoja na kujenga daraja la juu litakaloanzia eneo la Magomeni hadi njia panda ya Muhimbili (Fire) ambao umepangwa kuanza Februari 2024.
 
Serikali imesema wafanyakazi 279 waliokuwa wakifanya kazi na Kampuni ya Uendelezaji na Uendeshaji Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO) wataendelea kupata stahiki zao kama kawaida serikalini.

Novemba 10, KADCO ilikabidhi rasmi kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA) kwa mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA).

Hatua hiyo ilikuja kufuatia tamko la Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa alilolitoa Novemba 9 mwaka huu bungeni jijini Dodoma kufuatia mvutano uliodumu kwa mwaka mzima huku wabunge wakitaka TAA ichukue majukumu ya KADCO.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…