Makapuku Forum

Mwili wa Mwanaume mmoja ambaye jina lake halijafahamika umeopolewa maeneo ya Jangwani leo January 23,2024.

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shayo ameiambia @AyoTV_ kwamba walipata taarifa saa 3:45 asubuhi na walifika haraka kwa ajili ya uopoaji “Huyu aliyefariki ambaye mwili wake tumeuopoa ni Mwanaume ila hatujajua chanzo cha kifo chake ni kipi”
 
Mtoto mwingine ametolewa skrubu (screw) kwenye mapafu yake kwa kutumia kifaa chenye kamera katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es salaam baada ya kuimeza akiwa Shuleni.

Bingwa wa Magonjwa ya mapafu na mfumo wa upumuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Mwanaada Kilima, amesema Mtoto huyo alipaliwa na srew hiyo siku nne zilizopita ambayo iliyoingia kwenye mapafu yake na kumsababishia kukohoa sana huku jitihada za kuitoa kwa njia ya kawaida zikigonga mwamba.

Msafiri Chatanda ambaye ni Mzazi wa Mtoto huyo, amewashukuru watoa huduma wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa jitihada kubwa waliyofanya tangu alipofikishwa hospitalini hapo na kufanikisha kuitoa.

Katikati ya January hii kwa kutumia kifaa hicho, Jopo la Madaktari Bingwa wa upasuaji wa kifua, moyo, mapafu na mfumo wa upumuaji wa hospitali ya Taifa Muhimbili pia lilifanikiwa kuwasaidia Watu wengine wawili mmoja akiwa Mtoto wa miaka mitano aliyeondolewa shanga ya plastiki iliyokuwa imekwama katika pafu la kulia na mwingine ni Mwanamke (53) aliyeondolewa ganda la pipi kwenye pafu lake la kushoto alilodumu nalo kwa miaka 11.
 
[emoji187] Kwa sass tunakabiliwa na kazi kubwa ya kumfunga Mcongo halafu Zambia na Morocco watoke sare au Zambia wafungwe. Ni kazi ngumu. Ulazima wa kumfunga Congo ni moja kati ya kazi ngumu katika soka. Wanatuzidi mambo mengi kuanzia uwezo na hadhi ya mchezaji mmoja mmoja hadi kucheza kitimu. Wana timu haswa.
.
Walituonyesha tofauti yao na sisi kwa namna walivyokabiliana na Morocco. Wakati sisi tulikuwa wanyonge wao walionyesha ubora wao. Walichomoa bao na wakataka la ushindi. Na ni mechi ambayo inatia shaka kufikiria namna ambavyo pambano letu na Congo linavyoweza kwenda. Kama Fiston Mayele anaanzia benchi unaweza kufikiria ubora wa timu yao.
.
Vyovyote ilivyo tuanze kufikiria namna ya kushindana katika michuano ijayo. Hadi sasa inaonekana imeanza kuwa rahisi kuja katika michuano hii lakini bado tupo katika uwezo wa ushiriki tu na si ushindani. Tunahitaji kufanya uwekezaji wa kisasa katika soka.“ — Edo Kumwembe.
 
Farhan Jr Kihamu

Henock Inonga wa timu ya taifa ya Kongo ndio Inonga anayepaswa kuwepo kwenye uzi wa Simba, Inonga mtulivu sana wa Kongo anayefanya maamuzi mengi sahihi kwa wakati sahihi, Inonga asiyecheza na jukwaa, Inonga wa Kongo asiye na mambo mengi ndie anahitajika Simba, natamani sana Inonga wa Kongo ndie awe Inonga wa pale Msimbazi, ni Inonga wa maana sana.

Ila ukichunguza kiundani ni Wanaume anaocheza nao na presha ya kuvaa uzi wa Kongo ni tofauti na uzi wa Simba.
 
Farhan Jr Kihamu

Kuwa Captain na Staa wa nchi kama Mbwana Samatta kunakuja na gharama zake, yeye ni mwendelezo wa Mastaa wengi kwenye nchi zao ambao hubeba lawama hata kama hawastahili, game ya jana Captain kapika goli pekee, kafanya kazi kubwa mpaka kushuka chini kukaba ila bado watu watambebesha lawama, hii hutokana na ukubwa na mzigo ambao wakubwa hubebeshwa.

Haipo Tanzania tu bali duniani kote, utofauti tu ni kwamba watu wachache sana watakubali tuna Mbwana Samatta mmoja tu hatuna mwingine, pengine ndie Mchezaji wetu bora wa muda wote, ili afanye kile anachofanya Ulaya tunawahitaji Mbwana wengine wanne kila eneo, tunamtaka Mbwana wa Aston Villa, Genk, Paok ambaye hawezi kupatikana Tanzania.

All the best Captain Diego, real ones know the streets are watching[emoji123]

 
Farhan Jr Kihamu

MOHAMED HUSSEIN yes Marcelo wa Magomeni yupo kwenye kiwango bora sana kwasasa, maamuzi mengi sahihi, utulivu mkubwa na ni moja kati ya Wachezaji waliocheza kwa nidhamu sana siku ya jana, Mchezaji aliyeonesha uelewq mkubwa wa kimbinu, kushuka kwa wakati sahihi na kupanda kwa wakati sahihi, super game kutoka kwake[emoji123]

Bahati mbaya sana watu wanasubiri akosee aitwe Mzee.
 
G
Uwanja huu upo kwenye jiji la Yamoussoukro, ni miongoni mwa viwanja vipya vilivyojengwa maalum kwa ajili ya fainali za AFCON 2023, una uwezo wa kuchukua mashabiki 20,000 walioketi.

Umepewa jina la Charles Konan Banny Stadium [jina la Waziri Mkuu wa zamani wa Ivory Coast] ambaye alihudumu kati ya Disemba 2005 hadi Aprili 2007.

Charles Konan Banny alifariki kwa Covid-19 wakati janga hilo lilipoikumba dunia.

Kwenye mechi za makundi za AFCON 2023, uwanja huu unatumika kwa mechi za Kundi C [Senegal, Cameroon, Guinea na Gambia.
 
Kuwafunga wajomba zangu hiyo ni ndoto mnataka muote mchana kweupe
 
Timu ya taifa ya Ghana imekuwa na muendelezo mbaya kwenye mechi zake za hivi karibuni , mbali na kuondolewa kwa aibu kwenye Fainali za AFCON hapo jana bila ya ushindi wa mechi yoyote kwenye kundi lao.

Timu hiyo imecheza mechi 10 hadi kufikia jana na katika mechi hizo wamepata ushindi kwenye mechi moja tu kwenye mashindano ya AFCON kuanzia kufuzu hadi hapo jana .
 
Leopards
 
𝐅𝐔𝐋𝐋 𝐓𝐈𝐌𝐄 : Friendly

DALLAS FC 1-0 INTER MIAMI
[emoji460]️ 3” Fereirra

Hii ni usiku wa kuamkia leo ambapo Klabu ya Inter Miami imekumbana na kichapo cha bao 1-0 kutoka Kwa FC Dallas

Inter Miami Katika michezo miwili mfululizo ya kirafiki haijafunga Goli hata moja:

EL Salvador 0-0 Inter Miami
FC Dallas 1-0 Inter Miami

Kwenye mchezo huo Messi alitolewa dakika ya 64 baada ya upepo kukata timu ikiwa nyuma kwa bao 1-0
 
Askari wa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha, Sajenti Ismael Katenya (48), anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Manyara, akidaiwa kukutwa akisafirisha bunda 340 za dawa za kulevya aina ya mirungi.

Inadaiwa kuwa Katenya alikuwa anasafirisha bunda hizo 340 zinazokadiriwa kuwa ni kilo 140 alizozifunga kwenye magunia manne akitoka Arusha akielekea mkoani Mara.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi (ACP), George Katabazi akizungumza leo Januari 22, 2024 amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kamanda Katabazi amesema askari huyo alikamatwa Januari 22, 2024 saa 9 alasiri katika Mtaa wa Silaloda Tarafa ya Endagikot wilayani Mbulu.

Amesema Polisi huyo anadaiwa alikuwa anasafirisha dawa hizo za kulevya kwenye gari aina ya Nissan Patrol station wagon.

Amedai kuwa polisi huyo alifunga dawa hizo ndani ya magunia manne ambapo kila gunia moja alipakia bunda 50, bunda 40 zilikuwa ndani ya mfuko wa salfeti, bunda 87 zilikuwa kwenye begi jeusi kubwa na bunda 53 ndani ya begi dogo jeusi.
View attachment 2880823
 
Mshambuliaji wa timu ya Taifa Equatorial Guinea, Emilio Nsue ndiye mfungaji bora wa mashindano ya mataifa ya Afrika (Afcon) yanayofanyika nchini Ivory Coast.

Nsue (34) mwenye mabao matano baada ya michezo mitatu ya hatua ya makundi, pia ameiwezesha timu yake kumaliza kileleni mwa msimamo wa kundi A kwa pointi saba na kutinga hatua ya 16 bora.

Staa, aliyezaliwa Hispania na kunza maisha yake ya soka kwenye timu ya Real Mallorca ya nchini humo alikuwa kwenye kikosi cha vijana Hispania chini ya miaka 19 kilichotwaa kombe la Euro 2007.

Mshambuliaji huyo pia alicheza fainali za Euro 2011 katika kikosi kilichokuwa na mastaa wengine kama kiungo wa zamani wa Barcelona, Bayern Munic, Thiago Alcantara, Juan Mata and David de Gea, Dani Parejo.

Asili yake ni mzaliwa wa Equatorial Guinea alikozaliwa baba yake, huku mama yake akitokea Hispania.

 
Nuksi imeendelea kuiandama kambi ya timu ya taifa ya Misri inayoshiriki fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) zinazoendelea huko Ivory Coast, baada ya kipa wake chaguo la kwanza, Mohamed El Shenawy kupata majeraha yatakayomfanya akose mechi zote zilizobaki za mashindano hayo.

Shenawy amepata jeraha la bega katika dakika za nyongeza za mchezo baina ya Misri na Cape Verde uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 ambapo alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Mohamed Abou Gabal 'Gabanski'.

Jopo la matabibu wa Misri limetoa ripoti ya awali kuwa mchezaji huyo amepata tatizo la mfupa wa bega kuhama, hivyo kwa tathmini ya haraka, atahitajika kuwa nje ya uwanja kwa muda usiopungua miezi miwili.

Majeraha ya Shenawy yametokea katika muda usiozidi wiki moja tangu nyota wa Misri, Mohamed Salah alipopata maumivu ya misuli ambayo yatamuweka nje kwa wiki mbili.

 
Ushindi una raha yake bwana, hilo linathibitishwa na nchi ya Equatorial Guinea baada ya timu yao ya Taifa 'Nzalang Nacional' kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya timu mwenyeji wa fainali za mataifa ya Afrika (Afcon), Ivory Coast.

Rais wa nchi hiyo, Teodoro Obiang Nguema ametoa zawadi ya Euro 1 milioni (Sh 2.7 bilioni) kwa wachezaji na maofisa wa benchi la ufundi kama pongezi kwa ushindi huo.

Pia, ametangaza mapumziko ya siku moja leo Januari 23, 2024 kwa raia wa nchi yake ili kusherehekea ushindi huo.

Mabao manne ya Guinea katika mechi hiyo yalifungwa na Emilio Nsue aliyepachika mawili, Pablo Ganet na Jannick Buyla na yaliifanya timu yao imalize ikiwa kinara wa kundi A ikiwa imekusanya pointi saba na kutinga hatua ya 16 bora Afcon.

 
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa), limefunga kipande cha njia cha ‘Arrow Glacier’ ambacho hutumika na baadhi ya wageni wanaopanda Mlima Kilimanjaro kupitia njia ya Machame, Lemosho, Londorosi na Umbwe.

Taarifa za kufungwa kwa njia hizo, zimetolewa na Ofisa Uhifadhi Mwandamizi Kitengo cha Mawasiliano Tanapa, Catherine Mbena, huku ikieleza inatokana mvua zinazoendelea kunyesha katika mlima huo na kusababisha maporomoko ya mawe na miamba ya barafu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baada ya kusitisha matumizi ya kipande hicho, itatumika njia ya kawaida ya kutokea Baranco kelekea Karanga hadi kufika kileleni, hadi hapo mvua zitakapokoma na ukaguzi kufanyika, ili kujiridhisha kuwa njia hiyo ni salama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…