Makapuku Forum

Viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliofika eneo la Buguruni leo Jumatano asubuhi Januari 24, 2024 tayari kwa kuanza maandamano jijini Dar es Salaam.
 
STARS VITANI AFCON LEO
.
[emoji1241] TANZANIA [emoji739] DR CONGO [emoji1078]
[emoji354] 23:00
[emoji2522] Amadou Gon Coulibaly
.
Huu ni mchezo mgumu lakini Taifa Stars wakipambana vyema Ushindi unawezekana. Katika mashindano haya safari hii hakuna timu ndogo ni kujipanga tu hivyo kwa upande wetu, tunachohitaji ni ushindi ili tuweze kuingia katika hatua ya 16 Bora.
 
[emoji2788] “Hapa Liverpool wanafanya kazi ya usajili katika njia ya kipekee kabisa. Kabla ya kusajili tunafikiria mara mbili, tatu hadi nne. Unahitaji kuwa na uhakika wa kila kitu kwamba mchezaji huyo atakuja kufanya vizuri.

Sidhani kama kuna usajili wetu wowote mkubwa tuliofanya umekuja kufanya vibaya. Wakati mwingine mambo yanakuwa magumu kutokana na presha za watu. Na usipokuwa makini, basi utasajili kwa kuhamaki,” Jurgen Klopp, kocha wa Liverpool.
 
𝐅𝐔𝐋𝐋 𝐓𝐈𝐌𝐄 : AFCON
[emoji2522]GUINEA [emoji1119] 0-2 SENEGAL [emoji1211]

[emoji460]️ 61” Seck
[emoji460]️ 90” Ndiaye
𝐅𝐔𝐋𝐋 𝐓𝐈𝐌𝐄 : Afcon

[emoji2522]GAMBIA [emoji1108] 2-3 CAMEROON [emoji1062]
[emoji460]️ 72” Jallow
[emoji460]️ 85” Colley

[emoji460]️ 56” Ekambi
[emoji460]️ 87” Gomez (og)
[emoji460]️ 90+1” Wooh

[emoji1211] Senegal __________Pts 9
[emoji1062] Cameroon________Pts 4
[emoji1119] Guinea __________Pts 4
[emoji1108] Gambia __________Pts 1

Senegal na Cameroon wametinga 16 bora , Guinea anasubiri best loser Afcon
 
ZOEZI LA KUUTAFUTA MWILI WA KIJANA ALIYEJIRUSHA BAHARINI LAFUNGWA BILA MAFANIKIO

Kikosi Maalum cha kuzuia Magendo KMKM leo kimekamilisha na kufunga zoezi la utafutaji wa mwili wa kijana Mahmoud Mwalim aliyejirusha kwenye bahari wakati akiwa katika boti ya Zanzibar 3 iliyokuwa inatokea Pemba kwenda Unguja

Akizungumza na Wasafi Media Mkuu wa Operesheni KMKM Zanzibar Captain Hussein Mohamed Seif amesema zoezi hilo liloanza Januari 21, mwaka huu ambapo limedumu kwa siku tatu huku leo likitamatishwa kwa kuongezwa nguvu ya ziada ya kutandaza boti za utafutaji katika maeneo mbalimbali

Aidha amesema zoezi hilo limefungwa bila ya mafanikio yoyote huku wakiendelea kuwaomba wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka husika pindi watakapouona mwili huo

Amesema wanadhani mwili huo utakuwa umesogezwa ufukweni na maji hivyo ni vyema wananchi kutoa taarifa pindi watakapoona

 
Hahahahaha leo sijui niwe upande gani katika hii mechi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…