Musk apandikiza chip kwenye ubongo wa binadamu
Kampuni ya Neuralink inayomilikiwa na tajiri Elon Musk imefanikiwa kupandikiza kwa mara ya kwanza chip kwenye ubongo wa binadamu.
Mwezi wa 5 mwaka jana, Elon Musk alipata kibali kutoka FDA ya Marekani kuanza majaribio ya kifaa hicho kwa binadamu.
Majaribio hayo kwa binadamu yatadumu kwa miaka 6 kabla ya kuidhinishwa kutumika rasmi kwa binadamu iwapo kifaa hicho kinaonyesha mafanikio na kitakuwa salama.
Kampuni ya Neurolink imesema mgonjwa wa kwanza aliyepandikiziwa kifaa hicho kwenye ubongo anaendelea vizuri na chip hiyo imefanya kazi.
Wakati wa upandikizaji wa kifaa hicho Roboti zitakuwa zinatumika kupandikiza nyaya nyembamba kuliko nywele za binadamu kwenye ubongo wa binadamu.
Elon Musk anasema kifaa hicho ni kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa fahamu ikiwemo wagonjwa wenye stroke ambao sasa watakuwa wanaweza kuongea kupitia computer au simu.
Kwa sasa utafiti huo unafanyika kwa watu ambao wamekatika miguu na mikono..!