Makapuku Forum

Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Mzee Ali Hassan Mwinyi amepelekwa hospitali akiugua maradhi ya kifua.

Taarifa kwa umma iliyotolewa na msemaji wa familia, Abdullah Ali Mwinyi imeeleza kuwa, Rais huyo mstaafu, anaendelea kupata matibabu chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari.

Kutokana na ushauri wa madaktari wake, familia imeona ni vyema apate faragha akiwa anapatiwa matibabu. Hivyo familia inaiomba jamii kumkumbuka kwenye dua, swala na maombi, imesema taarifa hiyo iliyotolewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…