Meli ya Kampuni binafsi ya Flying Horse imezima ghafla ikiwa safarini kutoka Pemba kwenda Unguja na kusababisha taharuki kwa abiria.
Tukio hilo limetokea leo Fabruari 22, 2024 baada ya Injini moja ya kushoto kupata hitilafu muda mfupi kuanza safari yake
Akizungumza na Mwananchi Digital, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Baharini (ZMA), Sheikha Ahmed Mohamed amesema hitilafu hiyo imetokea dakika chache baada ya kutoka bandari ya Pemba.
“Kwahiyo ilikuwa haijatembea umbali mrefu na kilikuwa na meli zingine tulichofanya Serikali iliamrisha meli hizo ziivute kuirudisha bandarini Pemba bila kuleta madhara yoyote,” amesema
Mkurugenzi huyo, amesema abiria waliokuwa kwenye meli hiyo bila kutaja idadi yao, walihamishiwa kwenye meli nyinginezo zilizokuwa zinakwenda Unguja, Hivyo abiria walifika Salama na kuendelea na shughuli zao
Mmoja wa abiria aliyekuwamo kwenye meli hiyo, Makame Haji amesema meli hiyo ilikuwa haijatumia hata dakika tano, imetoka bandarini na ghafla walisikia ikibadilisha mgurumo na kupunguza mwendo
“Kilichosaidia bado tulikuwa karibu, watu wamepata hofu lakini haikuwa kubwa tulikuwa bado karibu na bandari,”
Ilikuja meli nyingie ikaivuta na kuirudisha kwenye gati tukashuka na kuhamishiwa kwenye meli nyingine tukaanza safari ya kuja Unguja,”