Makapuku Forum

RATIBA YA LEO IJUMAA

CAF CHAMPIONS LEAGUE
19:00 - Al Hilal [emoji1232] V/s Petero Atletico [emoji1029]
19:00 - Medeama SC [emoji1110] V/s Al Ahly [emoji1093]
22:00 - ASEC Mimosas [emoji1081] V/s Simba SC [emoji1241]

22:45 - Bologna V/s Hellas Verona
23:00 - Metz V/s Lyon
22:30 - Bayer Leverkusen V/s Mainz
23:00 - Real Sociaded V/s Villarreal
 
Ukipewa nafasi ya kutaja watu bora kwenye hicho unachofanya wewe mwenyewe utajiweka ______?

Kiungo wa Inter Milan Hakan Calhanoglu amesema yeye ndiyo kiungo namba moja duniani kwa sasa

β€œMimi ndio kiungo bora zaidi Duniani kwa sasa, Baada yangu ni Rodri ,Toni Kroos, Joshua Kimmich wa mwisho ni Enzo FernΓ‘ndez.”

1. Hakan
2.Rodri
3.Kroos
4.Kimmich
5.Enzo

Ameongeza kwa kusema yeye ni bora kwa sababu anafunga ila wengine wengi hawafungi na kwenye statistics anajisifu kuwa hafungi magoli ya karibu ni mashuti tu mita 25-30

30_______Mechi za msimu huu
11 _______Magoli
3 _______Assists
 
Siku moja iliyopita klabu ya Real Betis ilitangaza kukamilisha usajii wa mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya DRC Congo, Cedrix Bakambu aliyefanya vizuri kwenye Kombe la AFCON 2023

Usiku wa kuamkia leo kwenye UEFA Europa Conference League Bakambu amefunga goli lake la kwanza akiwa na klabu ya Real BΓ©tis na kufanya mechi iishe kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Zagreb
 
Kijiwe maarufu cha starehe kiitwacho Kitambaa Cheupe kilichopo Tabata Barakuda Jijini Dar es salaam kimeteketea kwa moto uliozuka mchana huu ambapo Jeshi la Zimamoto bado lipo eneo la tukio kuendelea kuzima moto huo ambao pia umezifikia hadi nguzo za umeme.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto ameahidi kuongea na @AyoTV_ muda mfupi ujao kutoa taarifa kamili kuhusu chanzo cha moto huo na taarifa nyingine muhimu kuhusu tukio zima, endelea kufuatilia kurasa za millardayo.
 
Duh..mbaya ingeungua ya Sinza
 
...nadhani ni kitendo kizuri sana. Mfungwa bado ni mtu na anapoondokewa na mtu wake wa karibu basi aruhusiwe kuhudhuria tahadhari zote zikichukuliwa. Sina hakika sana lakini kuna kesi moja (inawezekana alikuwa sio mfungwa tayari) lakini mama mmoja maarufu aliruhusiwa kwenda kuwazika wanaye ambao aliwapa sumu kisa mapenzi/wivu
 
Drc wana sheria mfungwa km una mke na ulijaza fomu basi mkeo anakaribishwa kukutembela mara moja kwa mwezi na mnatengewa chumba cha kuongea kikubwa na kushtua msuli kdg ..πŸ˜„πŸ˜„
 
Drc wana sheria mfungwa km una mke na ulijaza fomu basi mkeo anakaribishwa kukutembela mara moja kwa mwezi na mnatengewa chumba cha kuongea kikubwa na kushtua msuli kdg ..πŸ˜„πŸ˜„
...hii lazima ieleweke vizuri. Kwa tunaoruhusiwa mitala basi misuli itakuwa inashtuliwa kwa mtindo wa nne mara moja
 
Hali ilivyo ndani ya Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, baada mjane wa Bilionea Msuya pamoja na mwenzake kuachiwa huru.
 
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam inaendelea kusoma hukumu ya kesi ya mauaji inayomkabili mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini jijini Arusha, Erasto Msuya maarufu kama Bilionea Msuya, Miriam Mrita na mwenzake Revocatus Muyella maarufu kwa jina la Ray.

Kuhusu hoja ya gwaride la utambuzi kulingana na ushahidi ambao umeungwa mkono na mshahidi wengine, pia naitupilia mbali kuwa haina mashiko.

Kuhusu hoja ya kuwepo kwa mgongano wa nani aliandaa gwaride la utambuzi, ni kweli shahidi wa 13 alikiri kuwepo kwa mgongano huo kati ya ushahidi wake kizimbani na maelezo yake ya mandishi.

Hata hivyo maelezo hayo hayakuwasilishwa mahakamani ili Mahakama iweze kuona ubishani huo.

Hivyo Mahakama ilinyimwa nafasi ya kuona ukweli wa ubishani huo.

Hata hivyo ni msimamo kuwa lazima ushahidi wa utambuzi uwe umefanywa kwa mujibu wa sheria.

Ni maoni ya Mahakama hii kuwa kama kulikuwa na maswali aliyepaswa kuyajibu kama aliwasiliana na shahidi mtambuzi wa gwaride ni shahidi wa 10 ambaye ndiye aliyeandaa mashahidi, kama kabla ya gwaride alikuwa na mawasiliano na shahidi mtambuzi na si shahidi wa 13 ambaye yeye aliendesha tu gwaride.

Pia, sioni hoja ya msingi kuhusu shahidi wa 25 kushindwa kutambua alichokwenda kufanyia utambuzi.

 
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewaachia huru, mjane wa Bilionea Msuya, Miriam Mrita na Revocatus Muyella, baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao.
 
Revocatus Muyella amezungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, baada ya kuachiwa huru.

Muyella na mjane wa Bilionea Msuya, Miriam Mrita walikuwa wanakabiliwa na shitaka moja la mauaji kwa kudaiwa kumuua dada wa Bilionea Msuya, Aneth Msuya.
 
Askari wakimtuliza mmoja wa ndugu wa marehemu Aneth Msuya, Antujwa Msuya akilia baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salalam kutoa uamuzi wa kuwaachia huru mjane wa Bilionea Msuya, Miriam Mrita na mwenzake Revocatus Muyella.

Muyella na mjane wa Bilionea Msuya, Miriam Mrita walikuwa wanakabiliwa na shitaka moja la mauaji kwa kudaiwa kumuua dada wa Bilionea Msuya, Aneth Msuya.
 
Dada wa Aneth Msuya, Antujwa Msuya amesema mahakama haijatenda haki baada ya kutoa uamuzi wa kuwaachia huru mjane wa Bilionea Msuya, Miriam Mrita na mwenzake Revocatis Muyella.

Antujwa ametoa kauli hiyo leo Februari 23, 2024 baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Saalam kuwaachia huru wifi yake Miriam na Muyella waliokuwa wakikabiliwa na shitaka moja la mauaji ya Aneth Msuya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…