Makapuku Forum

Chad inafanya uchaguzi kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu ya utawala wa kijeshi, ikitazamiwa kuwa nchi ya kwanza barani Afrika inayoongozwa na jeshi kuhamia kwenye utawala wa kidemokrasia kwa kura za wananchi.

Nchi hiyo itamaliza kipindi cha mpito cha miaka mitatu kilichowekwa, baada ya kifo cha ghafla cha kiongozi wa muda mrefu, Idriss Deby Itno alipokuwa akipambana na waasi.

Jenerali Mahamat Déby ambaye ni mtoto wa kiongozi huyo, ni mmoja mwa watu wanaopendekezwa kushinda kiti hicho cha urais katika uchaguzi unaofanyika leo Mei 6, 2024.

Waziri Mkuu Succès Masra ni miongoni mwa wapinzani wake tisa, na anaonekana kuwa mpinzani wake mkubwa katika kinyang’anyiro hicho.

Wanasiasa wengine kumi ambao walikuwa na matumaini ya kugombea, wakiwemo watu wawili mashuhuri, Nassour Ibrahim Neguy Koursami na Rakhis Ahmat Saleh, walitengwa na baraza la katiba kwa sababu ya "ukiukaji taratibu".

Koursami aliyeshtakiwa kwa ulaghai, lakini wengine wamedai kuwa uamuzi wa kuwazuia watu fulani ulichochewa kisiasa.

Wanaharakati wametoa wito wa kususia uchaguzi huo, ambao waliutaja kuwa njama ya kutoa mwanga wa uhalali wa kidemokrasia kwa familia ya Deby.

Watu wengi bado wako uhamishoni wakisakwa vikali baada ya kufanya maandamano ya upinzani Oktoba 2022.

 
Jambo zuri sana ingawa baadhi wanalilalamikia.
Hesabu inaanza na moja, kama unataka kuhesabu mpaka alfu moja unatakiwa kuwa na subira.
Napongeza jeshi la nchi hiyo kwa uamuzi huo sahihi.
 
[emoji599] SAFARI YA INJINIA, LUBUMBASHI
.
YANGA imeanza kwa kasi mbio za usajili na safari hii haitaki kuambiwa, inapanda mwewe kujionea yenyewe ubora wa mastaa inaowataka, yaani kisasa zaidi na unavyosoma hili Rais wa klabu hiyo, Hersi Said yupo jijini Lubumbashi, DR Congo [emoji1078] akiwafuata mastaa wawili wapya.
.
Tuanze na juzi. Hersi alikuwa Uwanja wa Kibasa Maliba akitazama mchezo wa Ligi Kuu ya DR Congo Lubumbashi Sport dhidi ya TP Mazembe uliomalizika kwa suluhu. Kwenye mchezo huo Lubumbashi Sport anayoichezea beki wa zamani wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ikicheza soka la kujilinda ikainyima ushindi Mazembe na baada ya mchezo huo Hersi alifanya kikao kifupi na Ninja akitaka kufahamu maendeleo yake lakini ziara yake ikaendelea na jana akitua kwenye mchezo mwingine mgumu.
.
Jana Hersi akatua Uwanja wa Victoria kutazama mechi nyingine ya Ligi Kuu nchini humo kati ya AS Union Maniema dhidi ya FC Lupopo lakini Arena tunafahamu kigogo huyo aliyeibadili Yanga kwa hesabu kali za usajili aliwafuata mastaa wawili kutoka kwenye timu zote hizo.
 
Pale Union Maniema, Hersi alikuwa anajiridhisha juu ya ubora wa sasa wa winga Agee Basiala Amongo (25) ambaye ilibaki kidogo achukuliwe dirisha dogo la usajili lililopita. Basiala ni winga ambaye anahitajika na Kocha Miguel Gamondi na Yanga ilishamalizana naye na kumwacha hapo kwa sharti anatakiwa kupewa nafasi ya kucheza na yeye mwenyewe kutunza kipaji chake.
.
Gamondi anataka winga mpya kwa msimu ujao baada ya kutoridhishwa na kiwango cha Msauzi, Mahlatse Makudubela Skudu ambaye kwa vyovyote Yanga itamtema mwisho wa msimu huu.
.
Agee ni winga anayejua kupasua ukuta wa wapinzani kwa vyenga na kupiga krosi, pia ni mzuri wa kufunga kwa mipira ya adhabu ndogo kwa mguu wa kulia. Mbali na Basiala, pia Hersi kwa upande wa pili alikuwa na kazi ya kumtazama beki wa kushoto wa Lupopo…
.
Inaendelea …
 
Mbali na winga Agee Basiala, pia Rais wa Yanga, Hersi Said kwa upande wa pili alikuwa na kazi ya kumtazama beki wa kushoto wa Lupopo, Chadrack Boka ambaye Yanga inataka aje kuchukua nafasi ya Lomalisa Mutambala.
.
Boka ambayeni beki mrefu anayejua kupandisha mashambulizi na kuzuia, anahesabika kuwa beki bora wa kushoto na Mazembe inamtamani kila msimu lakini inajua haiwezi kumchukua kirahisi kwa kuwa ni watani wa jadi na Lupopo na hakuna biashara inayoweza kufanyika kati ya klabu hizo mbili.
.
Taarifa kutoka ndani ya Lupopo ni Yanga ilishabisha hodi ndani ya klabu yao ikimtaka Boka mwisho wa msimu huu, safari ambayo uhakika bosi huyo wa Yanga ametua huko kumaliza dili hilo. Endapo kila kitu kitaenda sawa basi Yanga haitakuwa na kazi ngumu kuwapata kwani mabosi wa klabu zote ni marafiki wakubwa na tajiri wa mabingwa hao wa Tanza-nia, Ghalib Said Mohammed ‘GSM’.
.
Union Maniema ina urafiki mkubwa na Yanga hatua ambayo hata Simba ilipofanya jaribio la kutaka kumsomba winga Maxi Nzengeli mchakato huo ulikwama kutokana na mawasiliano ya karibu ya Yanga na tajiri wa Maniema Generali wa Jeshi la Congo Amis Kumba. Kumba maarufu kwa jina la ‘Tango Four’ ndiye mmiliki wa Maniema na kabla kigogo huyo kichaa wa soka alikuwa rais wa AS Vita Club na baada ya kung’atuka kwake timu hiyo ikapotea.
 
[emoji187] “Takwimu zinatuonyesha Kevin De Bruyne ni bora kuliko Zinedine Zidane. Macho yetu yanatuambia Zidane ni bora kwa mbali kuliko staa huyu wa Manchester City na timu ya taifa ya Ubelgiji. Takwimu zinatuonyesha Cristiano Ronaldo ni bora kuliko Diego Maradona na Ronaldo De Lima. Hali halisi inatuambia hao wawili ni bora kuliko Ronaldo. Hapa ndipo linapoibuka suala la Kibu.
.
Hana mabao mengi lakini kuna kitu ambacho Simba wanakiona kwa Kibu kuliko kwa wachezaji wengine. Ukiwaambia Simba nani aondoke kati ya Kibu au Freddy Michael watakwambia Freddy aondoke ingawa ni huyu huyu amefunga mabao mengi kuliko Kibu. Soka la namba linatuchanganya katika dunia ya kisasa. Unajaribu kushindana na hali halisi. Hapa ndipo Kibu anapohitaji pesa nyingi katika mkataba wake. Hapo ndipo Kibu anadengua.” — Edo Kumwembe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…