Makapuku Forum

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema ili kuwezesha na kuimarisha huduma ya utoaji na upatikanaji wa mikopo kwa Wanafunzi wa elimu ya juu wenye sifa na uhitaji, Serikali itaongeza fursa za mikopo kwa Wanafunzi wa elimu ya juu kutoka 223,201 hadi 252,245.

Akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2024/2024, leo May 07,2024 Prof. Mkenda amesema “Serikali itatoa mikopo kwa Wanafunzi 84,500 wa mwaka wa kwanza ambapo shahada ya kwanza 80,000, shahada za juu 2,000, wanaosoma nje ya Nchi 500 na SAMIA Skolashipu 2,000, pia itatoa mikopo kwa Wanafunzi 157,745 wanaoendelea na masomo”

“Serikali pia itatoa ufadhili wa masomo kwa Wanafunzi 40 wenye ufaulu wa juu kwenye masomo ya sayansi hususan Wanafunzi wa kike waliohitimu Mtihani wa Taifa ya Kidato cha Sita na shahada ya awali kupitia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na itaanza kutoa ufadhili kwa ajili ya shahada za juu ikiwemo eneo la fani ya mionzi na nyuklia”
 
Katika mwaka wa fedha ujao (2024/2025), Serikali inatarajia kujenga karakana ya matengenezo ya ndege katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA). Chuo cha Usafirishaji Tanzania (NIT) ndicho kitakachotekeleza mradi huo.

Hayo yalibainishwa jana Mei 6, 2024 na Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025, bungeni jijini Dodoma.

Aidha Profesa Makame amesema NIT imeendelea kutekeleza miradi mingine ikiwemo ununuzi wa vifaa vya mafunzo ya urubani na uhandisi, matengenezo ya ndege, ikiwemo ‘flight simulators mbili’.

 
Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag amesema bado anataka kuendelea kupambana kuhakikisha anakuwa kocha wa timu hiyo msimu ujao pamoja na kupata matokeo mabaya.

United iliwashanga wengi jana baada ya kuchapwa mabao 4-0 na Crystal Palace kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliopigwa Uwanja wa Selhurst Park na sasa timu hiyo inatakiwa kuhakikisha inashinda michezo iliyobaki ili kurudisha matumaini.

Hata hivyo, mchezo unaofuata wa timu hiyo ni dhidi ya Arsenal ambayo inawania ubingwa wa Ligi Kuu England ambayo inataka kuhakikisha inapata ushindi ili kuendelea kuipa presha Man City ambayo nayo inawania ubingwa huo.

Kichapo cha juzi kimeifanya United kuweka rekodi ya kufungwa michezo mingi kwa msimu mmoja baada ya hadi sasa kupoteza 13, baada ya kuruhusu mabao 81 kwenye michuano yote ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 1977.

Ten Hag amesema timu yake imepoteza nguvu ya kupambana, lakini anatakiwa kufanya kazi kubwa kuhakikisha inaanza kushinda upya ikiwa imebakiza michezo mitatu imalize msimu.
 
Meya wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada amesema wanatarajia kujenga makumbusho ili kuhifadhi historia ambako Wajerumani wakati wa utawala wao walikuwa wakiwanyonga Wahehe waliomtii Chifu Mkwawa.

Eneo hilo, inasemekana kulikuwa na mti uliotumika kuwanyongea raia hao wenyeji na kuwa aliyefikishwa hapo alifungwa kitanzi shingoni na kuning'inizwa hadi kufa.

Neno ‘kitanzi’ ndilo lililozaa jina la mtaa na kata – Kitanzini – lilipo eneo hilo la kihistoria.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu, Ngwada amesema kutokana na historia hiyo wageni wengi hutembelea eneo hilo lenye ‘kitanzi’ ili kulishuhudia.

Amesema kutokana na kuwa kivutio hicho cha utalii, awali walijenga mnara wenye kitanzi lakini bahati mbaya ukawa katikati ya Barabara, kiasi cha kuzuia magari kupita.

"Sasa tunajenga pembeni na wazee wametuonyesha kilipokuwa kitanzi chenyewe, wapo ambao waliuona mti huo. Hapo ndio tutajenga makumbusho," amesema Ngwada.
 
Wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Kenya Airways waliokuwa wamekamatwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wameachiliwa huru.

Hayo yamethibitishwa jana Mei 6, 2024 na ofisa mwandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje Kenya.

Kitengo cha ujasusi wa kijeshi cha DRC kilizuia wafanyakazi wawili wa shirika hilo Aprili 19, mwaka huu kwa madai ya kukosa nyaraka za forodha kwenye baadhi ya mizigo ya thamani.

Wawili hao walizuiwa licha ya agizo la Mahakama kutaka waachiliwe.

Mmoja wa wafanyakazi hao ni raia wa Kenya na mwingine raia wa DRC.
 
Watu wanne wamefariki dunia na wengine 24 wameondolewa kwenye vifusi baada ya jengo kuporomoka katika mji wa George Afrika Kusini.

Jengo hilo limeporomoka jana Mei 6, 2024 huku wengine zaidi ya 50 wakiwa bado wamenaswa chini ya vifusi vya eneo la ujenzi.

Zaidi ya wafanyakazi 100 wa dharura na mbwa wa kunusa kwa sasa wako eneo la tukio wakitafuta manusura chini ya vifusi na kwenye matofali ya zege.

Wanafamilia walipiga kambi katika jengo la manispaa iliyo karibu ili kusubiri habari za jamaa zao.

Mamlaka ya eneo hilo imesema wafanyakazi 75 wa ujenzi walikuwa kwenye eneo la tukio wakati jengo la ghorofa tano likiporomoka huku sababu ya kuanguka kwa jengo hilo bado haijajulikana.
 
Vladimir Putin anatarajiwa kuapishwa leo Mei 7, 2024 kuendelea kuliongoza Taifa la Russia kwa kipindi kingine cha miaka sita huku akiwa ametawala kwa miaka 24.

Putin alishinda urais kwa asilimia 87.27 ya kura zote katika uchaguzi uliofanyika Machi mwaka huu, ikiwa ni baada ya kufanyika mabadiliko ya katiba yanayoruhusu aweze kugombea urais hadi mwaka 2036.

Kiongozi huyo anarejea katika utawala wakati ambao vita kati ya Russia na Ukraine iliyoanza Februari 24, 2022, ikifisha miaka miwili.

Uingereza na Canada zilisema hazitamtuma mtu yeyote kwenye sherehe hiyo, huku msemaji wa Umoja wa Ulaya ameliambia Shirika la Habari la Reuters kwamba balozi wa umoja huo Russia hatahudhuria sherehe hizo kwa kuzingatia msimamo wa nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Ulaya.

 
Habari wana JF

Matumaini yangu wote mko poa kabisa.

Uzi huu ni kwaajili ya wote. Lengo ni kujadili changamoto zinazotukabili, pia Kupeana support katika mambo yetu hapa JF. Tupeane mbinu za kukabiliana na mambo yote hum

Karibu sana
Nimepata kikokotoo changu milioni 40tsh naomba ushauri wa biashara nayo weza kufanya? Umri wangu ni miaka 50. Napenda Sana kilimo ila naogopa kutumbukia mafao yangu yote kwenye umri huu wa lala salama.
 
Mmmh? Uliamua kuniacha kwenye mataa siyo?
Shida ni kua Leo nimeshinda siku nzima kutafuta pesa.
Siwez kuacha kutafuta pesa kwa lunch.
Nishafika hapa tulipokutana first date, njoo uninunulie hiyo dinner thatha😂😂😂😂😂😂
 
Shida ni kua Leo nimeshinda siku nzima kutafuta pesa.
Siwez kuacha kutafuta pesa kwa lunch.
Nishafika hapa tulipokutana first date, njoo uninunulie hiyo dinner thatha😂😂😂😂😂😂
😳 Sasa mi saivi niko feri huku kayenze kesho nikuletee sato au sangara?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…