Serikali imetenga kiasi cha Tsh. bilioni 18.5 kwa ajili ya kuwawezesha Wajasiriamali Nchini zitakazotolewa kama mikopo yenye masharti nafuu kupitia Benki ya NMB (@nmbtanzania ).
Makubaliano ya utaratibu wa ufadhili huo yametiwa saini leo Jijini Dar es Salaam na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Seif Abdallah Shekalaghe kwa niaba ya Serikali na kushuhudiwa na Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Dorothy Gwajima.
Akiongea kabla ya utiaji saini ya mkataba huo wa miaka miwili, Waziri Gwajima amesema Wafanyabiashara wadogo na wa kati watakopeshwa fedha hizo kwa riba ya 7% “Tsh. bilioni 18.5 ni hela nyingi za kuanzia lakini kiasi hiki kitaongezeka kwani lengo la Serikali ni kuifanya mikopo hii kuwa endelevu ili iwafikide Watu wengi”
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna amesema mkataba wa kutoa mikopo hiyo ni kielelezo cha jitihada kubwa zinazofanywa na benki hiyo kuunga mkono juhudi za Serikali kuboresha mazingira ya biashara kwa Wafanyabiashara wote Nchini wakiwemo wadogo.
View attachment 2983795