Makaroni ya nyama na nazi

Makaroni ya nyama na nazi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Makaroni nichakula jamii ya Tambi,ni moja kati ya vyakula ambavyo napenda kupika siku za jumapili ninapokwepa kukaa jikoni kwa muda mrefu.
makaroni ya nyanya na nazi

Mahitaji

  • Makaroni mfuko 1
  • Njegere kikombe 1 ,osha acha zidondoshe maji
  • Vitunguu maji 3 vikubwa,kata vipande vidogo
  • Carry powder kijiko 1 cha chjakula
  • Pilau masala kijiko 1 cha chakula
  • Nyanya 4 kubwa ,saga na maganda yake
  • Nyanya ya kopo vijiko 2 vya chakula(tomato pest)
  • Vitunguu saumu kijiko 1 cha chakula,kata vipande vidogo
  • Karoti robo kikombe,kata vipande vidogo
  • Nazi paketi 2 (tumia Nazi ya Azam)
  • pilipilimanga robo kijiko cha chai
  • Blue band nusu kijiko cha chai
  • Mafuta yakupikia kwa kiasi upendacho


Njia
1.Chemsha maji yatokote,ongeza chumvi na makaroni,ivisha macaroni kasha chuja maji zibaki kavu.
3.Katika sufuria weka mafuta,vitunguu maji,carrypowder na pilau masala kanga pamoja adi vitunguu viive ,hakikisha haviungui.ongeza nyanya ya tunda na yakopo,vitunguu saumu kisha kaanga pamoja adi viive na nyanya ijitenge na mafuta ndani ya sufuria.
4.Punguza moto uwe mdogo,kisha ongeza Nazi uku ukikoroga mfululizo,fanya ivyo adi nyanya na Nazi viungane na kua uji mzito sana,Zima jiko vikiwa tayari

  • Ili kuongeza Nazi vizuri,weka Nazi kwenye kikombe na ongeza maji vijiko 4 vya chakula ndani yake,koroga adi Nazi iwe nyepesi ndipo ongeza kwenye nyanya
  • Muhimu kupunguza moto na kukoroga mfululizo ili Nazi isikatike na ili kuruhusu nyanya na Nazi kuungana na kua kama uji mzito sana
5.kisha ongeza makaroni,njegere,karoti na pilipili manga.changanya vizuri adi uji wote wa nyanya opotelee kwenye makaroni ,ongeza chumvi kwakiasi upendacho.
6.Chukua kaserola (bakuli la udongo ambalo unaweza kulitumia kuoka chakula) au chombo chochote unachoweza kutumia kuoka.kisha Pakaa blue band kwa ndani na mimina makaroni katika kaserola kisha oka kwenye oven kwa dakika 15 hadi 20 katika moto wa wastani,adi njegere na karoti zisinyae

  • Unaweza tumia sufuria au chombo chochote cha kuokea,ni vyema kutenga chakula hiki mezani kikiwa katika chombo ulichotumia kuoka,kugeuza chakula hiki kwenye chombo kingine hupunguza uzuri wa muonekano wake,nakufanya umbo lake zuri liharibike.

7.Makaroni tayari kabisa kwa kula,unaweza kula chakula hiki na mboga yoyote upendayo.Inapendeza zaidi ukila kabla hakijapoa.
 
shukrani kwa elimu. kinapendeza machoni nadhani mdomoni kitakuwa ni zaidi.
 
hii makitu nimepika jana aseeee tumejilambaa hatare,cjawai fikiria pilau masala-zanzibar nilitumia inakoleza mchuzi namna ile MziziMkavu santee niliprint kbs nikaweka mbele ya meza uku nakalangiza.
nikiweza upload pic nitatuma apa kwa mrejesho:A S wink:
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom