Wadau, hii mitandao ya simu imeona kuna fursa kubwa kwenye malipo ya mtandaoni hasa Kwa kutumia hizi virtual cards. Nimeshangaa Kuona bili ya Dola 17.2 zimekatwa elfu sitini na mbili yaani (62,000). Exchange rate ya 3647.
Jana hiii rate wametoa BOT au wapi. He BOT hawaoni kuna haja ya kuregulate hizi rate zisizo eleweka?
Wadau wenye uzoefu wa bank, je MAKATO yapoje?
Hii kitu imenikuta hivi juzi, nimelipa kwa Mpesa Visa card nimekatwa zaidi ya 10% ila bidhaa ileile nilijaribu kuinunua kwa DTB Mastercard makato yalikuwa kidogo sana.
Ni kweli kabisa hii ni huduma tuione kama dharula ila kama mtu upo siriaz na kazi unahitaji kufanya boosting social media muda wote haifai utaishia kutajirisha watu