Kila mteja wa PBZ anaetumia PBZ mobile ametumiwa ujumbe usemao: "Ndugu mteja, PBZ itaanza kutekeleza agizo la serikali la kutoza tozo kwa kila unapotoa pesa, kuanzia tarehe 01/07/2022. Asante kwa Ushirikiano"
Ujumbe huu umewafadhaisha wateja wengi wa PBZ na kujiona kuwa hata kile kipato chao kichache wanachokihifadhi huko benki kumbe nacho kishatazamwa na kudukuliwa.
Hapo nyuma mfanyakazi wa sekta ya umma hapa Zanzibar mshahara wake hulipwa katika eneo lake la kazi. Hata hivyo benki ya PBZ kutokana na maendeleo ya teknolojia ikashauriana na sekta za umma kuwa watumishi wote wapokelee mishahara yao kupitia benki.
Hili liekuja kutokana na usalama wa mishahara ya watumishi hao pamoja na kuiengezea benki kipato.
Na zaidi katika jambo hili ni msukumo wa benki yenyewe kwa ufupi ilitokana na ushawishi wa PBZ wakati walipo kosa nguvu za ushindani na mabenki mengine yalipojiekeza hapa Zanzibar na kujikuta PBZ wanapungukiwa na wateja. Ndio wakaweka mkakati wa kuishawishi serikali kulazimisha watumishi wake kuwalipa kupitia benki.
Jambo hili ni zuri kwa usalama wa mishahara ya watumishi. Kwani zimesharipotiwa taarifa nyingi za kuibiwa mishahara hio. Watumishi nao wakalifurahia suala hilo la kuhifadhiwa mishahara yao benki. Lakini kwa hili walilokujanalo serikali la kukata kiasi cha pesa katika mshahara wa mtumishi kila anapokwenda kutoa pesa yake benki limewahuzunisha watumishi wengi kwani wanaona hata kile kichache wanachopokea nacho kiwe kinapunguzwa.
Hivyo wanaiomba serikali waangalie njia mbadala ya kuongeza mapato na waondowe hio tozo katika mishahara ya watumishi. Ukizingatia mshahara huo tayari umeshakatwa kodi ya mapato (in come tax).