Makavu-Live forum

Wavulana wanatembea na Selfie Stick ila daima wanaume wanatembea na cheque book,wavulana wanatafuta sifa ili wasifiwe na warembo ila wanaume wanajenga heshima na kuitunza heshima,wavulana wanapost ujinga ila wanaume wanapost mawazo chanya yanayodumu milele kwa vizazi vijavyo.Wavulana wanauza viwanja ili wanunue magari la wanaume wanauza magari ili wanunue viwanja kwa ajili ya Investment ya kurithisha vizazi vyao.

Kuna tofauti kubwa sana ya kimawazo kati ya mwanaume na mvulana,mvulana hukimbia familia na kuitelekeza ila wanaume hubaki na kuitunza familia,wavulana hujikomba kwa watu maarufu na viongozi ila wanaume hujitenga na watu maarufu na viongozi ili kutengeneza jina lake kwa utashi wake na hazina ya maarifa yake na juhudi zake binasfi.Siku zote mwanaume hutafuta pesa kwa njia bora na sahihi na ufikapo muda wa kuvuna pesa hukaa ndani wakingojea pesa ije ndani,pesa inagonga mlango mwanaume anaamka anaifungulia mlango pesa na pesa inaingia ndani na anaikata miguu pesa inabaki ndani daima kwa ajili ya kuwekeza.

Kipimo cha utu uzima ni majukumu na sio umri sababu unaweza kuwa first born na usiyejua majukumu yako na ukawa last born na uakwa kichwa cha familia,hakikisha unatunza heshima yako sababu ukijiheshimu na wewe utaheshimiwa . Heshima mtu haombi ila anapewa heshima kulingana na haiba ,tabia na mwenendo wake. If you work hard, make good choices and excellent decisions, and do what you can do best, you are likely to be rewarded with a lucky future.
 
Zamani wanafunzi walikuwa wanatafuta vyuo vikuu na walipopata nafasi za vyuo walisomea utashi na weredi bila kusahau uungwana ,utu na ubunifu . siku hizi vyuo vinatafuta wanafunzi na wakipata wanafunzi hao wanafunzi wanasomea mitihani na kusomea mishahara na ndio maana kwa sasa malaya wanaojiuza ni wanafunzi wa vyuo vikuu,mashoga wapo vyuoni.

Serikali na makampui nao wanaajiri vyeti na sio utashi wa mtu.Unaweza ukawa na first class na usiwe lecture mzuri na unaweza kuwa na pass ya kawaida ukawa lecturer mzuri.Tizama kwenye soccial media jinsi wasomi walivyo na bikira za mawazo na uoga wa fikra .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…